Chapter 4
1 Yesu
alitoka katika mto Yordani akiwa amejaa Roho Mtakatifu, akaongozwa na Roho
mpaka jangwani.
2 Huko
alijaribiwa na Ibilisi kwa muda wa siku arubaini. Wakati huo wote hakula
chochote, na baada ya siku hizo akasikia njaa.
3 Ndipo
Ibilisi akamwambia, "Kama wewe ni Mwana wa Mungu, amuru jiwe hili liwe
mkate."
4 Yesu
akamjibu, "Imeandikwa: `Mtu haishi kwa mkate tu."`
5 Kisha
Ibilisi akamchukua hadi mahali pa juu, akamwonyesha kwa mara moja falme zote za
ulimwengu. Huyo Shetani akamwambia,
6
"Nitakupa uwezo juu ya falme zote hizi na fahari zake, kwa maana nimepewa
hivi vyote; nikitaka kumpa mtu ninaweza.
7 Hivi
vyote vitakuwa mali yako wewe, kama ukiniabudu."
8 Yesu
akamjibu, "Imeandikwa: `Utamwabudu Bwana Mungu wako, na utamtumikia yeye
peke yake."`
9 Ibilisi
akamchukua mpaka Yerusalemu, kwenye mnara wa Hekalu, akamwambia, "Kama
wewe ni Mwana wa Mungu,
10 kwa
maana imeandikwa: `Atawaamuru malaika wake wakulinde,`
11 na
tena, `Watakuchukua mikononi mwao usije ukajikwaa mguu wako kwenye jiwe."`
12 Lakini
Yesu akamjibu, "Imeandikwa: `Usimjaribu Bwana Mungu wako."`
13 Ibilisi
alipokwishamjaribu kwa kila njia, akamwacha kwa muda.
14 Yesu
alirudi Galilaya akiwa amejaa nguvu za Roho Mtakatifu, na habari zake zikaenea
katika sehemu zote za jirani.
15 Naye
akawa anawafundisha watu katika masunagogi yao, akasifiwa na wote.
16 Basi,
Yesu alikwenda Nazareti, mahali alipolelewa, na siku ya Sabato, aliingia katika
sunagogi, kama ilivyokuwa desturi yake. Akasimama ili asome Maandiko Matakatifu
kwa sauti.
17
Akapokea kitabu cha nabii Isaya, akakifungua na akakuta mahali palipoandikwa:
18
"Roho wa Bwana yu juu yangu, kwani amenipaka mafuta niwahubirie maskini
Habari Njema. Amenituma niwatangazie mateka watapata uhuru, vipofu watapata
kuona tena; amenituma niwakomboe wanaoonewa,
19 na
kutangaza mwaka wa neema ya Bwana."
20 Baada
ya kusoma, akafunga kile kitabu, akampa mtumishi, kisha akaketi; watu wote
wakamkodolea macho.
21 Naye
akaanza kuwaambia, "Andiko hili mlilosikia likisomwa, limetimia leo."
22 Wote
wakavutiwa sana naye, wakastaajabia maneno mazuri aliyosema. Wakanena,
"Je, huyu si mwana wa Yosefu?"
23 Naye
akawaambia, "Bila shaka mtaniambia msemo huu: `Mganga jiponye mwenyewe`,
na pia mtasema: `Yote tuliyosikia umeyafanya kule Kafarnaumu, yafanye hapa pia
katika kijiji chako."`
24
Akaendelea kusema, "Hakika nawaambieni, nabii hatambuliwi katika kijiji
chake.
25 Lakini, sikilizeni! Kweli kulikuwa na wajane wengi
katika nchi ya Israeli nyakati za Eliya. Wakati huo mvua iliacha kunyesha kwa
muda wa miaka mitatu na nusu; kukawa na njaa kubwa katika nchi yote.
26 Hata hivyo, Eliya hakutumwa kwa mjane yeyote ila kwa
mwanamke mjane wa Sarepta, Sidoni.
27 Tena, katika nchi ya Israeli nyakati za Elisha kulikuwa
na wenye ukoma wengi. Hata hivyo, hakuna yeyote aliyetakaswa ila tu Naamani,
mwenyeji wa Siria."
28 Wote waliokuwa katika lile sunagogi waliposikia hayo
walikasirika sana.
29 Wakasimama, wakamtoa nje ya mji wao uliokuwa umejengwa
juu ya kilima, wakampeleka mpaka kwenye ukingo wa kilima hicho ili wamtupe
chini.
30 Lakini Yesu akapita katikati yao, akaenda zake.
31 Kisha Yesu akashuka mpaka Kafarnaumu katika mkoa wa
Galilaya, akawa anawafundisha watu siku ya Sabato.
32 Wakastaajabia uwezo aliokuwa nao katika kufundisha.
33 Na katika lile sunagogi kulikuwa na mtu aliyekuwa
amepagawa na roho ya pepo mchafu; akapiga ukelele wa kuziba masikio:
34
"We! Yesu wa Nazareti! Kwa nini unatuingilia? Je, umekuja kutuangamiza? Ninakufahamu wewe ni
nani. Wewe ni mjumbe Mtakatifu wa Mungu!"
35 Lakini
Yesu akamkemea huyo pepo akisema: "Nyamaza! Mtoke mtu huyu!" Basi,
huyo pepo baada ya kumwangusha yule mtu chini, akamtoka bila kumdhuru hata
kidogo.
36 Watu
wote wakashangaa, wakawa wanaambiana, "Hili ni jambo la ajabu, maana kwa
uwezo na nguvu anawaamuru pepo wachafu watoke, nao wanatoka!"
37 Habari
zake zikaenea mahali pote katika mkoa ule.
38 Yesu
alitoka katika lile sunagogi, akaenda nyumbani kwa Simoni. Mama mmoja, mkwewe
Simoni, alikuwa na homa kali; wakamwomba amponye.
39 Yesu
akaenda akasimama karibu naye, akaikemea ile homa, nayo ikamwacha. Mara yule
mama akainuka, akawatumikia.
40 Jua
lilipokuwa linatua, wote waliokuwa na wagonjwa wao mbalimbali waliwaleta kwake;
naye akaweka mikono yake juu ya kila mmoja wao, akawaponya wote.
41 Pepo
waliwatoka watu wengi, wakapiga kelele wakisema: "Wewe u Mwana wa
Mungu!" Lakini Yesu akawakemea, wala hakuwaruhusu kusema, maana
walimfahamu kwamba yeye ndiye Kristo.
42 Kesho
yake asubuhi Yesu aliondoka akaenda mahali pa faragha. Watu wakawa wanamtafuta,
na walipofika mahali alipokuwa, wakajaribu kumzuia ili asiondoke kwao.
43 Lakini
yeye akawaambia, "Ninapaswa kuhubiri Habari Njema za Ufalme wa Mungu
katika miji mingine pia, maana nilitumwa kwa ajili hiyo."
44 Akawa
anahubiri katika masunagogi ya Yudea.
|