Chapter 14
1 Siku
moja ya Sabato, Yesu alikwenda kula chakula nyumbani kwa mmoja wa viongozi wa
Mafarisayo; watu waliokuwapo hapo wakawa wanamchunguza.
2 Mbele
yake Yesu palikuwa na mtu mmoja aliyekuwa na ugonjwa wa kuvimba mwili.
3 Yesu
akawauliza walimu wa Sheria na Mafarisayo, "Je, ni halali au la kumponya
mtu siku ya sabato?"
4 Lakini
wao wakakaa kimya. Yesu akamshika huyo mgonjwa, akamponya, akamwacha aende
zake.
5 Halafu
akawaambia, "Ni nani kati yenu ambaye mtoto wake au ng`ombe wake
akitumbukia shimoni, hangemtoa hata kama ni siku ya Sabato?"
6 Nao
hawakuweza kumjibu swali hilo.
7 Yesu
aliona jinsi wale walioalikwa walivyokuwa wanajichagulia nafasi za heshima,
akawaambia mfano:
8
"Kama mtu akikualika arusini, usiketi mahali pa heshima isije ikawa
amealikwa mwingine mheshimiwa kuliko wewe;
9 na
mwenyeji wenu ninyi wawili atakuja na kukwambia: `Mwachie huyu nafasi.` Hapo
utaaibika mbele ya wote na kulazimika kwenda kuchukua nafasi ya mwisho.
10 Bali
ukialikwa kwenye karamu, keti mahali pa mwisho, ili mwenyeji wako atakapokuja
akwambie: `Rafiki, njoo hapa mbele, mahali pazuri zaidi.` Hapo utakuwa
umeheshimika mbele ya wote wanaoketi pamoja nawe.
11 Kwa
maana yeyote anayejikweza atashushwa, na anayejishusha, atakwezwa."
12 Halafu
akamwambia na yule aliyemwalika, "Kama ukiwaandalia watu karamu mchana au
jioni, usiwaalike rafiki zako au jamaa zako au jirani zako walio matajiri,
wasije nao wakakualika nawe ukawa umelipwa kile ulichowatendea.
13 Badala
yake, unapofanya karamu, waalike maskini, vilema viwete na vipofu,
14 nawe
utakuwa umepata baraka, kwa kuwa hao hawana cha kukulipa. Maana Mungu atakupa
tuzo lako wakati watu wema watakapofufuka."
15 Mmoja
wa wale waliokuwa wameketi pamoja na Yesu akasema, "Ana heri mtu yule
atakayekula chakula katika Ufalme wa Mungu."
16 Yesu
akamjibu, "Mtu mmoja alifanya karamu kubwa, akaalika watu wengi.
17 Wakati
wa karamu ulipofika alimtuma mtumishi wake awaambie walioalikwa, `Njoni, kila
kitu ni tayari.`
18 Lakini
wote, kwa namna moja, wakaanza kuomba radhi. Wa kwanza akamwambia mtumishi:
`Nimenunua shamba, kwa hiyo sina budi kwenda kuliangalia; nakuomba uniwie
radhi.`
19
Mwingine akasema: `Nimenunua ng`ombe jozi tano wa kulima; sasa nimo njiani
kwenda kuwajaribu; nakuomba uniwie radhi.`
20 Na
mwingine akasema: `Nimeoa mke, kwa hiyo siwezi kuja.`
21
Mtumishi huyo akarudi na kumwarifu bwana wake jambo hilo. Yule mwenye nyumba
alikasirika, akamwambia mtumishi wake: `Nenda upesi kwenye barabara na
vichochoro vya mji, uwalete hapa ndani maskini, viwete, vipofu na waliolemaa.`
22
Baadaye, mtumishi huyo akasema: `Bwana mambo yamefanyika kama ulivyoamuru,
lakini bado iko nafasi.`
23 Yule
bwana akamwambia mtumishi: `Nenda katika barabara na vichochoro vya mji
uwashurutishe watu kuingia ili nyumba yangu ijae.
24 Kwa
maana, nawaambieni, hakuna hata mmoja wa wale walioalikwa atakayeonja karamu
yangu."`
25 Hapo,
makundi mengi yakawa yanaandamana pamoja na Yesu. Basi, akawageukia akawaambia,
26
"Mtu yeyote akija kwangu, asipowachukia baba na mama yake, mke wake,
watoto, ndugu na dada zake, naam, hata na nafsi yake mwenyewe, hawezi kuwa
mwanafunzi wangu.
27 Mtu
asipochukua msalaba wake na kunifuata hawezi kuwa mwanafunzi wangu.
28 Kwa
maana, ni nani miongoni mwenu ambaye akitaka kujenga mnara hataketi kwanza
akadirie gharama zake ili ajue kama ana kiasi cha kutosha cha kumalizia?
29 La
sivyo, baada ya kuweka msingi na kushindwa kumaliza, watu watamcheka
30
wakisema: `Mtu huyu alianza kujenga, lakini hakumalizia.`
31
"Au, ni mfalme gani ambaye, akitaka kwenda kupigana na mfalme mwingine,
hataketi kwanza chini na kufikiri kama ataweza, kwa askari wake elfu ishirini?
32 Kama
anaona hataweza, atawatuma wajumbe kutaka masharti ya amani wakati mfalme huyo
mwingine angali mbali.
33 Vivyo
hivyo, basi, hakuna hata mmoja wenu atakayekuwa mwanafunzi wangu kama
asipoachilia kila kitu alicho nacho.
34
"Chumvi ni nzuri; lakini ikipoteza ladha yake, itakolezwa na nini?
35 Haifai
kitu wala kwa udongo wala kwa mbolea. Watu huitupilia mbali. Sikieni basi, kama
mna masikio!"
|