Chapter 17
1 Kisha, Yesu akawaambia wanafunzi wake, "Haiwezekani
kabisa kusitokee vikwazo vinavyosababisha dhambi; lakini ole wake mtu yule
atakayevisababisha.
2 Ingekuwa afadhali kwake kufungiwa shingoni jiwe kubwa la
kusagia na kutoswa baharini, kuliko kumkwaza mmoja wa wadogo hawa.
3 Jihadharini! Kama ndugu yako akikukosea, mwonye; akitubu,
msamehe.
4 Na kama akikukosea mara saba kwa siku, na kila mara
akarudi kwako akisema `Nimetubu`, lazima umsamehe."
5 Mitume wakamwambia Bwana, "Utuongezee imani."
6 Naye Bwana akajibu, "Kama imani yenu ingekuwa ndogo
hata kama chembe ndogo ya haradali, mngeweza kuuambia mti huu wa mkuyu: `Ng`oka
ukajipandikize baharini`, nao ungewatii.
7 "Tuseme mmoja wenu ana mtumishi ambaye analima
shambani au anachunga kondoo. Je, anaporudi kutoka shambani, atamwambia:
`Haraka, njoo ule chakula?`
8 La! Atamwambia: `Nitayarishie chakula, ujifunge tayari
kunitumikia mpaka nitakapomaliza kula na kunywa, ndipo nawe ule na unywe.`
9 Je utamshukuru huyo mtumishi kwa sababu ametimiza
aliyoamriwa?
10 Hali kadhalika na ninyi mkisha fanya yote mliyoamriwa,
semeni: `Sisi ni watumishi tusio na faida, tumetimiza tu yale tuliyotakiwa
kufanya."`
11 Yesu akiwa safarini kwenda Yerusalemu alipitia mipakani
mwa Samaria na Galilaya.
12 Alipokuwa anaingia katika kijiji kimoja, watu kumi wenye
ukoma walikutana naye, wakasimama kwa mbali.
13 Wakapaza sauti wakisema, "Yesu Mwalimu, tuonee
huruma!"
14 Alipowaona akawaambia, "Nendeni mkajionyeshe kwa
makuhani." Basi, ikawa walipokuwa wanakwenda, wakatakasika.
15 Mmoja wao alipoona kwamba ameponywa alirudi akimtukuza
Mungu kwa sauti kubwa.
16 Akajitupa chini mbele ya miguu ya Yesu huku akimshukuru.
Huyo alikuwa Msamaria.
17 Hapo Yesu akasema, "Je, si watu kumi walitakaswa?
Wale tisa wako wapi?
18 Hakupatikana mwingine aliyerudi kumtukuza Mungu ila tu
huyu mgeni?"
19 Halafu akamwambia huyo mtu, "Simama, uende zako;
imani yako imekuponya."
20 Wakati mmoja, Mafarisayo walimwuliza Yesu, "Ufalme
wa Mungu utakuja lini?" Naye akawajibu, "Ufalme wa Mungu hauji kwa
namna itakayoweza kuonekana.
21 Wala hakuna atakayeweza kusema, `Uko hapa`, au `Uko
pale`. Kwa kweli Ufalme wa Mungu uko kati yenu."
22 Halafu akawaambia wanafunzi wake, "Siku zinakuja
ambapo mtatamani kuona mojawapo ya siku za Mwana wa Mtu, lakini hamtaiona.
23 Na watu watawaambieni: `Tazameni yuko hapa`; ninyi
msitoke wala msiwafuate.
24 Kwa maana kama vile umeme unavyotokea ghafla na kuangaza
anga upande mmoja hadi mwingine, ndivyo Mwana wa Mtu atakavyokuwa siku yake.
25 Lakini kabla ya hayo, itambidi ateseke sana na
kukataliwa na kizazi hiki.
26 Kama ilivyokuwa nyakati za Noa, ndivyo itakavyokuwa
katika siku za Mwana wa Mtu.
27 Watu waliendelea kula na kunywa, kuoa na kuolewa mpaka
wakati ule Noa alipoingia katika safina. Gharika ikatokea na kuwaangamiza wote.
28 Itakuwa kama ilivyotokea wakati wa Loti. Watu waliendelea kula na kunywa,
kununua na kuuza, kupanda mbegu na kujenga.
29 Lakini
siku ile Loti alipoondoka Sodoma, moto na kiberiti vikanyesha kama mvua kutoka
mbinguni na kuwaangamiza wote.
30 Ndivyo
itakavyokuwa siku ile Mwana wa Mtu atakapofunuliwa.
31
"Siku hiyo, yeyote atakayekuwa juu ya paa asishuke nyumbani kuchukua mali
yake. Kadhalika, naye atakayekuwa shambani asirudi nyuma.
32
Kumbukeni yaliyompata mke wa Loti.
33 Yeyote
anayetaka kuiokoa nafsi yake, ataipoteza; na yeyote anayeipoteza, ataiokoa.
34 Nawaambieni,
siku ile usiku watu wawili watakuwa wanalala pamoja, mmoja atachukuliwa na yule
mwingine ataachwa.
35
Wanawake wawili watakuwa wakisaga nafaka pamoja; mmoja atachukuliwa na mwingine
ataachwa."*fc* atachukuliwa na mwingine ataachwa.\ie
36 missing
37 Hapo
wakamwuliza, "Ni wapi Bwana?" Naye akawaambia, "Ulipo mzoga,
ndipo tai watakapokusanyikia."
|