Chapter 8
1 Saulo naye alikiona kitendo hicho cha kumwua Stefano kuwa
sawa. Siku hiyo kanisa la Yerusalemu lilianza kuteswa vibaya. Waumini wote,
isipokuwa tu wale mitume, walilazimika kutawanyika katika sehemu za mashambani
za Yudea na Samaria.
2 Watu wamchao Mungu, walimzika Stefano na kumfanyia
maombolezo makubwa.
3 Wakati huohuo, Saulo alijaribu kuliangamiza kanisa.
Alikwenda katika kila nyumba, akawatoa nje waumini, wanaume kwa wanawake,
akawatia gerezani.
4 Wale waumini waliotawanyika, walikwenda kila mahali
wakihubiri ule ujumbe.
5 Naye Filipo aliingia katika mji wa Samaria na kumhubiri
Kristo kwa wenyeji wa hapo.
6 Watu walijiunga kusikiliza kwa makini ule ujumbe wa
Filipo na kuona ile miujiza aliyoifanya.
7 Maana pepo wachafu waliokuwa wamewapagaa watu wengi
waliwatoka wakipiga kelele kubwa; na pia watu wengi waliokuwa wamepooza viungo
na waliolemaa waliponywa.
8 Kukawa na furaha kubwa katika mji ule.
9 Basi, kulikuwa na mtu mmoja aitwaye Simoni ambaye alikuwa
amekwisha fanya uchawi wake katika mji huo kwa muda na kuwashangaza watu wa
Samaria, akijiona kuwa yeye ni mtu maarufu.
10 Watu wote, wadogo na wakubwa, walimsikiliza kwa makini
wakisema, "Simoni ndiye ile nguvu ya kimungu inayoitwa `Nguvu
Kubwa."`
11 Walivutiwa sana naye kwa vile alikuwa amewashangaza kwa
uchawi wake kwa muda mrefu.
12 Lakini walipouamini ujumbe wa Filipo juu ya Habari Njema
ya Ufalme wa Mungu na jina la Yesu Kristo, walibatizwa, wanawake na wanaume.
13 Hata Simoni aliamini; baada ya kubatizwa ilikuwa
akiandamana na Filipo, akastaajabia maajabu na miujiza iliyokuwa inafanyika.
14 Wale mitume waliokuwa kule Yerusalemu walipopata habari
kwamba wenyeji wa Samaria nao wamelipokea neno la Mungu, waliwatuma kwao Petro
na Yohane.
15 Walipofika waliwaombea hao waumini ili wampokee Roho
Mtakatifu;
16 maana wakati huo Roho Mtakatifu hakuwa ameshukia yeyote
kati yao; walikuwa wamebatizwa tu kwa jina la Bwana Yesu.
17 Basi, Petro na Yohane wakawawekea mikono hao waumini,
nao wakampokea Roho Mtakatifu.
18 Hapo Simoni aling`amua kwamba kwa kuwekewa mikono ya
mitume waumini walipewa Roho Mtakatifu. Hivyo aliwapa Petro na Yohane fedha
akisema,
19 "Nipeni na mimi uwezo huo ili yeyote nitakayemwekea
mikono, apokee Roho Mtakatifu."
20 Lakini Petro akamjibu, "Potelea mbali na fedha zako
kwa vile unafikiri kwamba unaweza kununua karama ya Mungu kwa fedha!
21 Huna sehemu yoyote wala haki katika kazi hiyo kwa maana
moyo wako hauko sawa mbele ya macho ya Mungu.
22 Kwa hiyo, tubu ubaya wako huu na umwombe Bwana naye
anaweza kukusamehe fikira kama hizo.
23 Ni dhahiri kwangu kwamba umejaa wivu mkali na mfungwa wa
dhambi!"
24 Simoni akajibu, "Tafadhali, niombeeni kwa Bwana
lisije likanipata lolote kati ya hayo mliyosema."
25 Baada ya Petro na Yohane kutoa ushuhuda wao na
kuutangaza ujumbe wa Bwana, walirudi Yerusalemu. Walipokuwa wanarudi walihubiri
Habari Njema katika vijiji vingi vya Samaria.
26 Malaika wa Bwana alimwambia Filipo, "Jitayarishe
uende kusini kupitia njia inayotoka Yerusalemu kwenda Gaza." (Njia hiyo
hupita jangwani.)
27 Basi, Filipo akajiweka tayari, akaanza safari. Wakati
huohuo kulikuwa na Mwethiopia mmoja, towashi, ambaye alikuwa anasafiri kuelekea
nyumbani. Huyo mtu alikuwa ofisa maarufu wa hazina ya Kandake, malkia wa
Ethiopia. Alikuwa amekwenda huko Yerusalemu kuabudu na wakati huo alikuwa
anarudi akiwa amepanda gari la kukokotwa.
28 Alipokuwa anasafiri, alikuwa akijisomea kitabu cha nabii
Isaya.
29 Basi, Roho Mtakatifu akamwambia Filipo, "Nenda
karibu na gari hilo ukafuatane nalo."
30 Filipo akakimbilia karibu na gari, akamsikia huyo mtu
akisoma katika kitabu cha nabii Isaya. Hapo Filipo akamwuliza, "Je,
unaelewa hayo unayosoma?"
31 Huyo mtu akamjibu, "Ninawezaje kuelewa bila mtu
kunielewesha?" Hapo akamwalika Filipo apande juu, aketi pamoja naye.
32 Basi, sehemu ya Maandiko Matakatifu aliyokuwa anasoma
ilikuwa hii: "Alikuwa kama kondoo anayepelekwa kuchinjwa; kimya kama vile
mwana kondoo anaponyolewa manyoya, yeye naye hakutoa sauti hata kidogo.
33 Alifedheheshwa na kunyimwa haki. Hakuna atakayeweza
kuongea juu ya kizazi chake, kwa maana maisha yake yameondolewa duniani."
34 Huyo Mwethiopia akamwambia Filipo, "Niambie, huyu
nabii anasema juu ya nani? Anasema mambo haya juu yake yeye mwenyewe au juu ya
mtu mwingine?"
35 Basi, Filipo akianzia na sehemu hiyo ya Maandiko
Matakatifu, akamweleza Habari Njema juu ya Yesu.
36 Walipokuwa bado wanaendelea na safari walifika mahali
penye maji na huyo ofisa akasema, "Mahali hapa pana maji; je, kuna
chochote cha kunizuia nisibatizwe?"*fa*
37 missing
38 Basi, huyo ofisa akaamuru lile gari lisimame; na wote
wawili, Filipo na huyo ofisa wakashuka majini, naye Filipo akambatiza.
39 Walipotoka majini Roho wa Bwana akamfanya Filipo
atoweke. Na huyo Mwethiopia hakumwona tena; lakini akaendelea na safari yake
akiwa amejaa furaha.
40 Filipo akajikuta yuko Azoto, akapita katika miji yote
akihubiri Habari Njema mpaka alipofika Kaisarea. kubatizwa." Naye akajibu,
"Naam, ninaamini kwamba Yesu Kristo ni Mwana wa Mungu."
|