Chapter 19
1 Wakati
Apolo alipokuwa Korintho, Paulo alisafiri sehemu za bara, akafika Efeso ambako
aliwakuta wanafunzi kadhaa.
2
Akauliza, "Je, mlipopata kuwa waumini mlipokea Roho Mtakatifu?" Nao
wakamjibu, "La! Hata kusikia kwamba kuna Roho Mtakatifu hatujasikia."
3 Naye
akasema, "Sasa mlipata ubatizo wa namna gani?" Wakamjibu,
"Ubatizo wa Yohane."
4 Naye
Paulo akasema, "Ubatizo wa Yohane ulikuwa wa kuonyesha kwamba watu
wametubu. Yohane aliwaambia watu wamwamini yule ambaye alikuwa anakuja baada
yake, yaani Yesu."
5 Baada ya
kusikia hayo, walibatizwa kwa jina la Bwana Yesu.
6 Basi,
Paulo akawawekea mikono, na Roho Mtakatifu akawashukia, wakaanza kusema lugha
mbalimbali na kutangaza ujumbe wa Mungu.
7 Wote
jumla, walikuwa watu wapatao kumi na wawili.
8 Kwa muda
wa miezi mitatu Paulo alikuwa akienda katika sunagogi, akawa na majadiliano ya
kuvutia sana juu ya Ufalme wa Mungu.
9 Lakini
wengine walikuwa wakaidi, wakakataa kuamini, wakaanza kuongea vibaya hadharani
juu ya Njia ya Bwana. Hapo Paulo alivunja uhusiano nao, akawachukua pembeni
wale wanafunzi wake, akawa anazungumza nao kila siku katika jumba la masomo la
Turano.
10
Aliendelea kufanya hivyo kwa muda wa miaka miwili hata wakazi wote wa Asia,
Wayahudi na watu wa mataifa mengine, wakaweza kusikia neno la Bwana.
11 Mungu
alifanya miujiza ya ajabu kwa mikono ya Paulo.
12 Watu
walikuwa wakichukua leso na nguo nyingine za kazi ambazo Paulo alikuwa
amezitumia, wakazipeleka kwa wagonjwa, nao wakaponywa magonjwa yao; na wale
waliokuwa na pepo wabaya wakatokwa na pepo hao.
13
Wayahudi kadhaa wenye kupunga pepo wabaya, walisafiri huko na huko, wakijaribu
kulitumia jina la Bwana Yesu kwa wale waliokuwa wamepagawa na pepo wabaya.
Walikuwa wakisema: "Ninawaamuru kwa jina la Yesu ambaye Paulo
anamhubiri."
14 Watoto
saba wa Skewa, Kuhani Mkuu wa Kiyahudi, walikuwa miongoni mwa hao waliokuwa
wanafanya hivyo.
15 Lakini
pepo mbaya aliwajibu, "Ninamfahamu Yesu, ninamjua pia Paulo, lakini ninyi
ni nani?"
16 Kisha
yule mtu aliyepagawa aliwarukia wote kwa kishindo, akawashinda nguvu. Na hao
watoto wa Skewa wakakimbia kutoka ile nyumba wakiwa uchi na wamejaa majeraha.
17 Kila
mtu huko Efeso, Myahudi na asiye Myahudi, alisikia juu ya tukio hilo. Wote
waliingiwa na hofu, wakalitukuza jina la Bwana Yesu.
18 Waumini
wengi walijitokeza wakakiri hadharani mambo waliyokuwa wametenda.
19 Wengine
waliokuwa wameshughulikia mambo ya uchawi hapo awali, walikusanya vitabu vyao,
wakavichoma mbele ya wote. Walikisia gharama ya vitabu hivyo, wakaona yafikia
vipande vya fedha elfu hamsini.
20 Kwa
namna hiyo, neno la Bwana lilizidi kuenea na kuwa na nguvu zaidi.
21 Baada
ya mambo hayo, Paulo aliamua kwenda Yerusalemu kwa kupitia Makedonia na Akaya.
Alisema, "Baada ya kufika huko, itanilazimu kuona Roma pia."
22 Hivyo,
aliwatuma wawili wa wasaidizi wake, Timotheo na Erasto, wamtangulie kwenda
Makedonia, naye akabaki kwa muda huko Asia.
23 Wakati
huo ndipo kulipotokea ghasia kubwa huko Efeso kwa sababu ya hiyo Njia ya Bwana.
24
Kulikuwa na mfua fedha mmoja aitwaye Demetrio, ambaye alikuwa na kazi ya
kutengeneza sanamu za nyumba ya mungu wa kike aitwaye Artemi. Shughuli hiyo
iliwapatia mafundi faida kubwa.
25
Demetrio aliwakusanya hao wafanyakazi pamoja na wengine waliokuwa na kazi kama
hiyo, akawaambia, "Wananchi, mnafahamu kwamba kipato chetu kinatokana na
biashara hii.
26 Sasa, mnaweza
kusikia na kujionea wenyewe mambo Paulo anayofanya, si tu hapa Efeso, ila pia
kote katika Asia. Yeye amewashawishi na kuwageuza watu wakakubali kwamba miungu
ile iliyotengenezwa na watu si miungu hata kidogo.
27 Hivyo
iko hatari kwamba biashara yetu itakuwa na jina baya. Si hivyo tu, bali pia
jambo hilo linaweza kuifanya nyumba ya mungu Artemi kuwa si kitu cha maana.
Hatimaye sifa zake huyo ambaye Asia na dunia yote inamwabudu, zitakwisha."
ic
28
Waliposikia hayo, waliwaka hasira, wakaanza kupiga kelele: "Mkuu ni
Artemi, wa Efeso!"
29 Mji
wote ukajaa ghasia. Wakawavamia Gayo na Aristarko, wenyeji wa Makedonia, ambao
walikuwa wasafiri wenzake Paulo, wakakimbia nao mpaka kwenye ukumbi wa michezo.
30 Paulo
mwenyewe alitaka kuukabili huo umati wa watu, lakini wale waumini walimzuia.
31 Maofisa
wengine wa huo mkoa wa Asia, waliokuwa rafiki zake, walimtumia Paulo ujumbe
wakimsihi asijihatarishe kwa kwenda kwenye ukumbi wa michezo.
32 Wakati
huo, kila mtu alikuwa anapayuka; wengine hili na wengine lile, mpaka hata ule
mkutano ukavurugika. Wengi hawakujua hata sababu ya kukutana kwao.
33 Kwa
vile Wayahudi walimfanya Aleksanda ajitokeze mbele, baadhi ya watu katika ule
umati walidhani kuwa ndiye. Basi, Aleksanda aliwaashiria watu kwa mkono akitaka
kujitetea mbele ya ule umati wa watu.
34 Lakini
walipotambua kuwa yeye ni Myahudi, wote kwa sauti moja walipiga kelele:
"Mkuu ni Artemi wa Efeso!" Wakaendelea kupayukapayuka hivyo kwa muda
wa saa mbili.
35
Hatimaye karani wa mji alifaulu kuwanyamazisha, akawaambia, "Wananchi wa
Efeso, kila mtu anajua kwamba mji huu wa Efeso ni mlinzi wa nyumba ya mungu
Artemi na mlinzi wa ile sanamu iliyoanguka kutoka mbinguni.
36 Hakuna
anayeweza kukana mambo haya. Hivyo basi, tulieni; msifanye chochote bila
hadhari.
37
Mmewaita watu hawa hapa ingawaje hawakuikufuru nyumba ya mungu wala kumtukana
mungu wetu wa kike.
38 Kama,
basi Demetrio na wafanyakazi wake wana mashtaka yao kuhusu watu hawa, yapo
mahakama na wakuu wa mikoa; wanaweza kushtakiana huko.
39 Kama
mna matatizo mengine, yapelekeni katika kikao halali.
40 Kwa
maana tungaliweza kushtakiwa kwa kusababisha ghasia kutokana na vituko vya leo.
Ghasia hii haina msingi halali na hatungeweza kutoa sababu za kuridhisha za
ghasia hiyo."
41 Baada
ya kusema hayo aliuvunja mkutano.
|