Chapter 21
1
Tulipokwisha agana nao, tulipanda meli tukaenda moja kwa moja mpaka Kosi. Kesho yake
tulifika Rodo, na kutoka huko tulikwenda Patara.
2 Huko,
tulikuta meli iliyokuwa inakwenda Foinike, hivyo tulipanda, tukasafiri.
3 Baada ya
kufika mahali ambapo tuliweza kuona Kupro, tulipitia upande wake wa kusini
tukaelekea Siria. Tulitia nanga katika mji wa Tiro ambapo ile meli ilikuwa
ipakuliwe shehena yake.
4 Tulikuta
waumini huko, tukakaa pamoja nao kwa muda wa juma moja. Waumini hao wakawa
waongea kwa nguvu ya Roho, wakamwambia Paulo asiende Yerusalemu.
5 Lakini
muda wetu ulipokwisha tuliondoka. Wote pamoja na wanawake na watoto wao
walitusindikiza mpaka nje ya mji. Tulipofika pwani, sote tulipiga magoti
tukasali.
6 Kisha
tuliagana; sisi tukapanda meli nao wakarudi makwao.
7 Sisi
tuliendelea na safari yetu kutoka Tiro tukafika Tolemai ambapo tuliwasalimu
ndugu zetu, tukakaa nao siku moja.
8 Kesho
yake tuliondoka tukaenda Kaisarea. Huko Kaisarea tulikwenda nyumbani kwa
mhubiri Filipo. Yeye alikuwa mmoja wa wale saba waliochaguliwa kule Yerusalemu.
9 Alikuwa
na binti watatu ambao walikuwa na kipaji cha unabii.
10 Baada
ya kukaa huko siku kadhaa, nabii mmoja aitwaye Agabo alifika kutoka Yudea.
11
Alitujia, akachukua mkanda wa Paulo, akajifunga mikono na miguu, akasema
"Roho Mtakatifu asema hivi: `Wayahudi kule Yerusalemu watamfunga namna hii
mtu mwenye ukanda na kumtia mikononi mwa watu wa mataifa."`
12
Tuliposikia hayo, sisi na wale watu wengine waliokuwa hapo tulimsihi Paulo
asiende Yerusalemu.
13 Lakini
yeye alijibu, "Mnataka kufanya nini? Mnataka kuvunja moyo wangu kwa
machozi? Niko tayari siyo tu kutiwa ndani kule Yerusalemu, ila hata kufa kwa
ajili ya Bwana Yesu."
14
Tuliposhindwa kumshawishi tulinyamaza, tukasema tu: "Mapenzi ya Bwana
yafanyike"
15 Baada
ya kukaa pale kwa muda, tulifunga mizigo yetu, tukaendelea na safari kwenda
Yerusalemu.
16 Wengine
kati ya wale wafuasi wa Kaisarea walienda pamoja nasi, wakatupeleka nyumbani
kwa Mnasoni ambaye tulikuwa tunakwenda kukaa naye kwa muda. Mnasoni alikuwa
mwenyeji wa Kupro na alikuwa amekuwa muumini kwa siku nyingi.
17
Tulipofika Yerusalemu, ndugu waumini walitupokea vizuri sana.
18 Kesho
yake Paulo alikwenda pamoja nasi kumwamkia Yakobo, na wazee wote wa kanisa
walikuwako pia.
19 Baada
ya kuwasalimu, Paulo aliwapa taarifa kamili kuhusu yote Mungu aliyokuwa
ametenda kati ya mataifa kwa njia ya utumishi wake.
20
Waliposikia hayo, walimtukuza Mungu. Kisha wakamwambia Paulo, "Ndugu,
unaweza kuona kwamba kuna maelfu ya Wayahudi ambao sasa wamekuwa waumini na
wote hao wanashika kwa makini Sheria ya Mose.
21
Wamepata habari zako kwamba umekuwa ukiwafundisha Wayahudi wanaoishi kati ya
mataifa mengine kuwa wasiijali Sheria ya Mose, wasiwatahiri watoto wao na
kwamba wasizifuate mila za Wayahudi.
22 Sasa,
mambo yatakuwaje? Ni dhahiri kuwa watapata habari kwamba umekwisha wasili hapa.
23 Basi, fanya kama tunavyokushauri. Tunao hapa watu wanne
ambao wameweka nadhiri.
24 Jiunge nao katika ibada ya kujitakasa, ukalipe na
gharama zinazohusika, kisha wanyolewe nywele zao. Hivyo watu wote watatambua
kwamba habari zile walizoambiwa juu yako hazina msingi wowote, na kwamba wewe
binafsi bado unaishi kufuatana na maagizo ya Sheria za Mose.
25 Kuhusu wale watu wa mataifa mengine ambao wamekuwa
waumini, tumekwisha wapelekea barua tukiwaambia mambo tuliyoamua: wasile chochote
kilichotambikiwa miungu ya uongo, wasinywe damu, wasile nyama ya mnyama
aliyenyongwa, na wajiepushe na uasherati."
26 Basi, kesho yake Paulo aliwachukua wale watu akafanya
ibada ya kujitakasa pamoja nao. Kisha akaingia Hekaluni kutoa taarifa kuhusu
mwisho wa siku za kujitakasa na kuhusu dhabihu itakayotolewa kwa ajili ya kila
mmoja wao.
27 Wakati siku hizo saba zilipokaribia kuisha, Wayahudi
waliokuwa wametoka katika mkoa wa Asia walimwona Paulo Hekaluni. Wakachochea hasira
kati ya kundi lote la watu, wakamtia nguvuni
28 wakipiga kelele: "Wananchi wa Israeli, msaada,
msaada! Huyu ndiye yule mtu anayewafundisha watu kila mahali mambo yanayopinga
watu wa Israeli, yanayopinga Sheria ya Mose na mahali hapa patakatifu. Hata
sasa amewaingiza watu wa mataifa mengine Hekaluni na kupatia najisi mahali hapa
patakatifu."
29 Sababu ya kusema hivyo ni kwamba walikuwa wamemwona
Trofimo mwenyeji, wa Efeso, akiwa pamoja na Paulo mjini, wakadhani kwamba Paulo
alikuwa amemwingiza Hekaluni.
30 Mji wote ulienea ghasia; watu wakaja kutoka pande zote,
wakamkamata Paulo, wakamburuta, wakamtoa nje ya Hekalu na papo hapo milango ya
Hekalu ikafungwa.
31 Walikuwa tayari kumuua, lakini habari zilimfikia mkuu wa
jeshi la Kiroma kuwa Yerusalemu yote ilikuwa imejaa ghasia.
32 Mara, mkuu wa jeshi akawachukua askari na jemadari,
akalikabili lile kundi la watu. Nao walipomwona mkuu wa jeshi na askari,
wakaacha kumpiga Paulo.
33 Mkuu wa jeshi alimwendea Paulo, akamtia nguvuni na
kuamuru afungwe minyororo miwili. Kisha akauliza, "Ni mtu gani huyu, na
amefanya nini?"
34 Wengine katika lile kundi la watu walikuwa wanapayuka
kitu hiki na wengine kitu kingine. Kwa sababu ya ghasia hiyo, mkuu wa jeshi
hakufaulu kujua kisa kamili. Hivyo, aliamuru watu wake wampeleke Paulo ndani ya
ngome.
35 Paulo alipofika kwenye ngazi, askari walilazimika
kumbeba kwa sababu ya fujo za watu.
36 Kwa maana kundi kubwa la watu walimfuata wakipiga
kelele, "Muulie mbali!" ic
37 Walipokuwa wanamwingiza ndani ya ngome, Paulo alimwomba
mkuu wa jeshi akisema, "Naweza kukwambia kitu?" Yule mkuu wa jeshi
akamjibu, "Je unajua Kigiriki?
38 Kwani wewe si yule Mmisri ambaye hivi majuzi alianzisha
uasi na kuwaongoza majahili elfu nne hadi jangwani?"
39 Paulo akajibu, "Mimi ni Myahudi, mzaliwa wa Tarso
katika Kilikia; mimi ni raia wa mji maarufu. Tafadhali, niruhusu niongee na
watu.
40 Yule mkuu wa jeshi akamruhusu. Hivyo Paulo alisimama juu
ya ngazi, akawapungia mkono wale watu na walipokaa kimya, akaanza kuongea nao
kwa Kiebrania.
|