Chapter 24
1 Baada ya siku tano, Kuhani Mkuu Anania aliwasili Kaisarea
pamoja na wazee kadhaa na wakili mmoja wa sheria aitwaye Tertulo. Walimwendea
yule mkuu wa mkoa wakamweleza mashtaka yao juu ya Paulo.
2 Paulo aliitwa na Tertulo akafungua mashtaka hivi:
"Mheshimiwa Felisi, uongozi wako bora umeleta amani kubwa na marekebisho
ya lazima yanafanywa kwa manufaa ya taifa letu.
3 Tunalipokea jambo hili kwa furaha daima na kutoa shukrani
nyingi kwako kila mahali.
4 Lakini, bila kupoteza wakati wako zaidi, tunakusihi kwa
wema wako, usikilize taarifa yetu fupi.
5 Tumegundua kwamba mtu huyu ni wa hatari mno. Yeye
huanzisha ghasia kati ya Wayahudi kila mahali duniani na pia ni kiongozi wa
kile chama cha Wanazareti.
6 Tena alijaribu kulikufuru Hekalu nasi tukamtia nguvuni.
Kama ukimhoji wewe mwenyewe, utaweza kubainisha mambo haya yote tunayomshtaki
kwayo."*fc*
7 missing
8 missing
9 Nao Wayahudi waliunga mkono mashtaka hayo wakisema kwamba
hayo yote yalikuwa kweli. jeshi, aliingilia kati, akamchukua kwa nguvu kutoka
mikononi mwetu. 8 Kisha akaamuru washtaki wake waje mbele yako.
10 Basi, mkuu wa mkoa alimwashiria Paulo aseme. Naye Paulo
akasema, "Nafurahi kujitetea mbele yako nikijua kwamba umekuwa hakimu wa
taifa hili kwa miaka mingi.
11 Unaweza kujihakikishia kwamba si zaidi ya siku kumi na
mbili tu zimepita tangu nilipokwenda kuabudu Yerusalemu.
12 Wayahudi hawakunikuta nikijadiliana na mtu yeyote.
Hawakunikuta nikichochea watu Hekaluni wala katika masunagogi yao, wala mahali
pengine popote katika mji huo.
13 Wala hawawezi kuthibitisha mashtaka waliyotoa juu yangu.
14 Ninachokubali mbele yako ni hiki: Mimi ninamwabudu Mungu
na wazee wetu nikiishi kufuatana na Njia ile ambayo wao wanaiita chama cha
uzushi. Ninaamini mambo yote yaliyoandikwa katika vitabu vya Sheria na manabii.
15 Mimi namtumainia Mungu, na wao wanalo tumaini hilo,
kwamba watu, wema na wabaya, watafufuka.
16 Kwa hiyo ninajitahidi daima kuwa na dhamiri njema mbele
ya Mungu na mbele ya watu.
17 "Baada ya kukaa mbali kwa miaka kadhaa, nilirudi
Yerusalemu ili kuwapelekea wananchi wenzangu msaada na kutoa dhabihu.
18 Wakati nilipokuwa nikifanya hayo ndipo waliponikuta
Hekaluni, nilipokuwa nimekwisha fanya ile ibada ya kujitakasa. Hakukuwako kundi
la watu wala ghasia.
19 Lakini kulikuwa na Wayahudi wengine kutoka mkoa wa Asia;
hao ndio wangepaswa kuwa hapa mbele yako na kutoa mashtaka yao kama wana
chochote cha kusema dhidi yangu.
20 Au, waache hawa walio hapa waseme kosa waliloliona
kwangu wakati niliposimama mbele ya Baraza lao kuu,
21 isipokuwa tu maneno haya niliyosema niliposimama mbele
yao: `Mnanihukumu leo hii kwa sababu ya kushikilia kwamba wafu
watafufuliwa!"`
22 Hapo, Felisi, ambaye mwenyewe alikuwa anaifahamu hiyo
Njia vizuri, aliahirisha kesi hiyo. Akawaambia, "Nitatoa hukumu juu ya
kesi hiyo wakati Luisa, mkuu wa jeshi, atakapokuja hapa."
23 Kisha akamwamuru yule jemadari amweke Paulo kizuizini,
lakini awe na uhuru kiasi, na rafiki zake wasizuiwe kumpatia mahitaji yake.
24 Baada ya siku chache, Felisi alifika pamoja na mkewe
Drusila ambaye alikuwa Myahudi. Aliamuru Paulo aletwe, akamsikiliza akiongea
juu ya kumwamini Yesu Kristo.
25 Lakini wakati Paulo alipoanza kuongea juu ya uadilifu,
juu ya kuwa na kiasi na juu ya siku ya hukumu inayokuja, Felisi aliogopa,
akasema, "Kwa sasa unaweza kwenda; nitakuita tena nitakapopata
nafasi."
26 Wakati huohuo alikuwa anatumaini kwamba Paulo angempa
fedha. Kwa sababu hii alimwita
Paulo mara kwa mara na kuzungumza naye.
27 Baada
ya miaka miwili, Porkio Festo alichukua nafasi ya Felisi, akawa mkuu wa Mkoa.
Kwa kuwa alitaka kujipendekeza kwa Wayahudi, Felisi alimwacha Paulo kizuizini.
|