Chapter 25
1 Siku
tatu baada ya kufika mkoani, Festo alitoka Kaisarea, akaenda Yerusalemu.
2 Makuhani
wakuu pamoja na viongozi wa Wayahudi walimpa habari kuhusu mashtaka yaliyokuwa
yanamkabili Paulo. Walimsihi Festo
3
awafanyie fadhili kwa kumleta Paulo Yerusalemu; walikuwa wamekula njama wamuue
akiwa njiani.
4 Lakini
Festo alijibu, "Paulo atabaki kizuizini kule Kaisarea na mimi nitakwenda
huko karibuni.
5 Waacheni
viongozi wenu waende huko pamoja nami wakatoe mashtaka yao juu yake kama
amefanya chochote kiovu."
6 Festo
alikaa nao kwa muda wa siku nane au kumi hivi, kisha akarudi Kaisarea. Kesho
yake alikwenda barazani, akaamuru Paulo aletwe ndani.
7 Wakati
Paulo alipofika, Wayahudi waliokuwa wametoka Yerusalemu walimzunguka wakaanza
kutoa mashtaka mengi mazitomazito ambayo hawakuweza kuthibitisha.
8 Kwa
kujitetea, Paulo alisema, "Mimi sikufanya kosa lolote kuhusu Sheria ya
Wayahudi, wala kuhusu Hekalu, wala kumhusu Kaisari."
9 Festo
alitaka kujipendekeza kwa Wayahudi na hivyo akamwuliza Paulo, "Je,
ungependa kwenda Yerusalemu na huko ukahukumiwe mbele yangu kuhusu mashtaka
haya?"
10 Paulo
akajibu, "Nasimama mbele ya mahakama ya Kaisari na papa hapa ndipo
ninapopaswa kupewa hukumu. Kama unavyojua vizuri, sikuwatendea Wayahudi ubaya
wowote.
11 Basi,
ikiwa nimepatikana na kosa linalostahili adhabu ya kifo, siombi kusamehewa
adhabu hiyo. Lakini kama hakuna ukweli katika mashtaka waliyotoa watu hawa,
hakuna awezaye kunikabidhi kwao. Nakata rufani kwa Kaisari!"
12 Basi,
baada ya Festo kuzungumza na washauri wake, akamwambia Paulo, "Umekata
rufani kwa Kaisari, basi, utakwenda kwa Kaisari."
13 Siku
chache baadaye, mfalme Agripa na Bernike walifika Kaisarea ili kutoa heshima
zao kwa Festo.
14
Walikuwa huko siku kadhaa naye Festo akamweleza mfalme kesi ya Paulo:
"Kuna mtu mmoja hapa ambaye Felisi alimwacha kizuizini.
15
Nilipokwenda Yerusalemu makuhani wakuu na wazee wa Wayahudi walimshtaki na
kuniomba nimhukumu.
16 Lakini
mimi niliwajibu kwamba si desturi ya Waroma kumtoa mtu aadhibiwe kabla
mshtakiwa hajakutana na washtaki wake ana kwa ana na kupewa fursa ya kujitetea
kuhusu hayo mashtaka.
17 Basi,
walipofika hapa sikukawia, ila nilifanya kikao mahakamani kesho yake, nikaamuru
mtu huyo aletwe.
18 Washtaki
wake walisimama lakini hawakutoa mashtaka maovu kama nilivyokuwa ninatazamia.
19 Ila tu
walikuwa na mabishano kadhaa pamoja naye kuhusu dini yao na kuhusu mtu mmoja
aitwaye Yesu ambaye alikufa, lakini Paulo anashikilia kwamba yu hai.
20 Sikujua
la kufanya kuhusu shauri hilo. Basi, nilimwuliza Paulo kama angependa kwenda
mahakamani kule Yerusalemu kwa ajili ya mashtaka hayo.
21 Lakini
Paulo alikata rufani, akaomba aachwe kizuizini mpaka uamuzi wa shauri hilo
ufanywe na Kaisari. Kwa hiyo niliamua akae kizuizini mpaka nitakapoweza
kumpeleka kwa Kaisari."
22 Basi
Agripa akamwambia Festo, "Ningependa kumsikia mtu huyu mimi
mwenyewe." Festo akamwambia, "Utamsikia kesho."
23 Hivyo,
kesho yake, Agripa na Bernike walifika kwa shangwe katika ukumbi wa mkutano
wakiwa wameandamana na wakuu wa majeshi na viongozi wa mji. Festo aliamuru
Paulo aletwe ndani,
24 Kisha
akasema, "Mfalme Agripa na wote mlioko hapa pamoja nasi! Hapa mbele yenu
yuko mtu ambaye jumuiya yote ya Wayahudi hapa na kule Yerusalemu
walinilalamikia wakipiga kelele kwamba hastahili kuishi tena.
25 Lakini
mimi sikuona kuwa alikuwa ametenda chochote kibaya hata astahili kupewa adhabu
ya kifo. Lakini, kwa vile Paulo mwenyewe alikata rufani kwa Kaisari, niliamua
kumpeleka.
26 Kwa
upande wangu sina habari kamili ambayo naweza kumwandikia Kaisari juu yake.
Ndiyo maana nimemleta hapa mbele yenu na mbele yako mfalme Agripa, ili baada ya
kumchunguza, niweze kuwa na la kuandika.
27 Kwa
maana nadhani itakuwa kichekesho kumpeleka mfungwa bila kutaja wazi mashtaka
yanayomkabili."
|