Chapter 16
1 Napenda kumjulisha kwenu dada yetu Foibe ambaye ni
mtumishi katika kanisa la Kenkrea.
2 Mpokeeni kwa ajili ya Bwana kama iwapasavyo watu wa
Mungu. Mpeni msaada wowote atakaohitaji kutoka kwenu, maana yeye amekuwa mwema
sana kwa watu wengi na kwangu pia.
3 Salamu zangu ziwafikie Priska na Akula, wafanyakazi
wenzangu katika utumishi wa Kristo Yesu.
4 Wao walihatarisha maisha yao kwa ajili yangu. Wanastahili
shukrani; si tu kutoka kwangu, bali pia kutoka kwa makanisa yote ya watu wa
mataifa mengine.
5 Salamu zangu pia kwa kanisa linalokutana nyumbani kwao.
Salamu zangu zimfikie rafiki yangu Epaineto ambaye ni kwa kwanza katika mkoa wa
Asia kumwamini Kristo.
6 Nisalimieni Maria ambaye amefanya kazi kwa bidii kwa
ajili yenu.
7 Salamu zangu kwa Androniko na Yunia, wananchi wenzangu
waliofungwa gerezani pamoja nami; wao wanajulikana sana kati ya mitume; tena
walikuwa Wakristo kabla yangu mimi.
8 Salamu zangu kwa Ampliato, rafiki yangu katika kuungana
na Bwana.
9 Salamu zangu zimfikie Urbano, mfanyakazi mwenzangu katika
utumishi wa Kristo; salamu zangu pia kwa rafiki yangu Staku.
10 Nisalimieni Apele ambaye uaminifu wake kwa Kristo
umethibitishwa. Salamu zangu kwa wote walio nyumbani mwa Aristobulo.
11 Salamu zangu kwa Herodiana, mwananchi mwenzangu; na kwa
jamaa yote ya Narkisi iliyojiunga na Bwana.
12 Nisalimieni Trufena na Trufosa wanaofanya kazi katika
utumishi wa Bwana, na rafiki yangu Persi ambaye amefanya mengi kwa ajili ya
Bwana.
13 Nisalimieni Rufo, mtu hodari sana katika kazi ya Bwana,
na mama yake ambaye ni mama yangu pia.
14 Nisalimieni Asunkrito, Flegoni, Herme Patroba, Herma na
ndugu wote walio pamoja nao.
15 Nisalimieni Filologo na Yulia, Nerea na dada yake, na
Olumpa, pamoja na watu wote wa Mungu walio pamoja nao.
16 Salimianeni ninyi kwa ninyi kwa ishara ya upendo. Salamu
kwenu kutoka kwa makanisa yote ya Kristo.
17 Ndugu zangu, nawasihi muwafichue wote wanaosababisha
mafarakano na kuwafanya watu wengine waanguke, kinyume cha mafundisho
mliyofundishwa. Jiepusheni na watu hao,
18 maana watu wa namna hiyo hawamtumikii Kristo Bwana wetu,
bali wanayatumikia matumbo yao wenyewe. Kwa maneno yao matamu na hotuba za
kubembeleza hupotosha mioyo ya watu wanyofu.
19 Kila mtu amesikia juu ya utii wenu na hivyo mmekuwa
sababu ya furaha yangu. Nawatakeni muwe na hekima katika mambo mema, na bila
hatia kuhusu mambo mabaya.
20 Naye Mungu aliye chanzo cha amani hatakawia kumponda
Shetani chini ya miguu yenu. Neema ya Bwana wetu Yesu Kristo iwe nanyi.
21 Timotheo, mfanyakazi mwenzangu, anawasalimu. Hali
kadhalika Lukio, Yasoni, na Sosipatro, wananchi wenzangu, wanawasalimu.
22 Nami Tertio, ninayeandika barua hii nawasalimuni katika
Bwana.
23 Gayo, mwenyeji wangu, pamoja na kanisa lote linalokutana
kwake, anawasalimu. Erasto, mweka hazina wa mji huu, pamoja na Kwarto,
wanawasalimu.*fb*
24 missing
25 Basi, sasa na tumsifu Mungu! Yeye anaweza kuwaimarisheni
katika ile Habari Njema niliyohubiri juu ya ujumbe wa Yesu Kristo, na katika
ile siri iliyofunuliwa na ambayo ilikuwa imefichika kwa karne nyinyi
zilizopita.
26 Lakini, sasa ukweli huo umefunuliwa kwa njia ya maandiko
ya manabii; na kwa amri ya Mungu wa milele umedhihirisha kwa mataifa yote ili
wote waweze kuamini na kutii.
27 Kwake Mungu aliye peke yake mwenye hekima, uwe utukufu
kwa njia ya Yesu Kristo, milele na milele! Amina.
|