Chapter 4
1 Mtu na
atuone sisi kuwa ni watumishi wa Kristo tuliokabidhiwa siri za mungu.
2
Kinachotakiwa kwa yeyote yule aliyekabidhiwa kazi ni kuwa mwaminifu.
3 Kwangu mimi
si kitu nikihukumiwa na ninyi, au na mahakama ya kibinadamu; wala sijihukumu.
4 Dhamiri
yangu hainishtaki kwa jambo lolote, lakini hiyo haionyeshi kwamba sina lawama.
Bwana ndiye anayenihukumu.
5 Basi,
msihukumu kabla ya wakati wake acheni mpaka Bwana atakapokuja. Yeye atayafichua
mambo ya giza yaliyofichika, na kuonyesha wazi nia za mioyo ya watu. Ndipo kila
mmoja atapata sifa anayostahili kutoka kwa Mungu.
6 Ndugu,
hayo yote niliyosema juu ya Apolo na juu yangu, ni kielelezo kwenu: kutokana na
mfano wangu mimi na Apolo nataka mwelewe maana ya msemo huu: "Zingatieni
yaliyoandikwa." Kati yenu pasiwe na mtu yeyote anayejivunia mtu mmoja na
kumdharau mwingine.
7 Nani amekupendelea wewe? Una kitu gani wewe ambacho
hukupewa? Na ikiwa umepewa, ya nini kujivunia kana kwamba hukukipewa?
8 Haya,
mmekwisha shiba! Mmekwisha kuwa matajiri! Mmekuwa wafalme bila ya sisi! Naam,
laiti mngekuwa kweli watawala, ili nasi pia tuweze kutawala pamoja nanyi.
9 Nafikiri
Mungu ametufanya sisi mitume tuwe watu wa mwisho kabisa, kama watu
waliohukumiwa kuuawa, maana tumekuwa tamasha mbele ya ulimwengu wote, mbele ya
malaika na watu.
10 Sisi ni
wapumbavu kwa ajili ya Kristo, lakini ninyi ni wenye busara katika kuungana na
Kristo! Sisi ni dhaifu, ninyi ni wenye nguvu. Ninyi mnaheshimika, sisi
tunadharauliwa.
11 Mpaka
dakika hii, sisi tuna njaa na kiu, hatuna nguo, twapigwa makofi, hatuna malazi.
12 Tena
twataabika na kufanya kazi kwa mikono yetu wenyewe. Tukitukanwa, tunawatakia
baraka; tukidhulumiwa, tunavumilia;
13
tukisingiziwa, tunajibu kwa adabu. Mpaka sasa tumetendewa kama uchafu wa dunia;
na kwa kila mtu sisi ni takataka!
14
Siandiki mambo haya kwa ajili ya kuwaaibisha ninyi, bali kwa ajili ya
kuwafundisheni watoto wangu wapenzi.
15 Maana
hata kama mnao maelfu ya walezi katika maisha yenu ya Kikristo, baba yenu ni
mmoja tu, kwani katika maisha ya Kikristo mimi ndiye niliyewazaeni kwa
kuihubiri Habari Njema.
16 Kwa
hiyo, nawasihi: fuateni mfano wangu.
17 Ndiyo
maana nimemtuma Timetheo kwenu. Yeye ni mtoto wangu mpenzi na mwaminifu katika
Bwana. Atawakumbusheni njia ninayofuata katika kuishi maisha ya Kikristo; njia
ninayofundisha kila mahali katika makanisa yote.
18 Baadhi
yenu wameanza kuwa na majivuno wakidhani kwamba sitakuja tena kwenu.
19 Lakini,
Bwana akipenda, nitakuja kwenu upesi; na hapo ndipo nitakapojionea mwenyewe,
sio tu kile wanachoweza kusema hao wenye majivuno, bali pia kila wanachoweza
kufanya.
20 Maana Utawala wa Mungu si shauri la maneno matupu, bali
ni nguvu.
21
Mnapendelea lipi? Nije kwenu na fimbo, ama nije na moyo wa upendo na upole?
|