Chapter 9
1 Je, mimi si mtu huru? Je, mimi si mtume? Je, mimi sikumwona
Yesu Bwana wetu? Je, ninyi si matokeo ya kazi yangu kwa ajili ya Bwana?
2 Hata kama kwa watu wengine mimi si mtume, lakini walau
kwenu ninyi mimi ni mtume. Ninyi ni uthibitisho wa mtume wangu kwa sababu ya
kuungana kwenu na Bwana.
3 Hoja yangu kwa wale wanaonipinga ndiyo hii:
4 Je, hatuna haki ya kula na kunywa?
5 Je, hatuna ruhusa kumchukua mke Mkristo katika ziara
zetu, kama vile wafanyavyo mitume wengine, ndugu zake Bwana, na pia Kefa?
6 Au ni mimi tu na Barnaba ambao tunapaswa kujipatia
maslahi yetu kwa kufanya kazi?
7 Je, mwanajeshi gani anayelipia utumishi wake jeshini?
Mkulima gani asiyekula matunda ya shamba lake la mizabibu? Mchungaji gani
asiyekunywa maziwa ya mifugo yake?
8 Je,
nasema mambo haya kibinadamu tu? Je, Sheria nayo haisemi hivyo?
9
Imeandikwa katika Sheria ya Mose: "Usimfunge kinywa ng`ombe anapoliwata
nafaka." Je, ndio kusema Mungu anajishughulisha na ng`ombe?
10 Je,
hakuwa anatufikiria sisi aliposema hivyo? Naam, haya yaliandikwa kwa ajili
yetu; kwani yule anayelima na yule anayevuna, wote wawili wana haki ya
kutumaini kupata sehemu ya mavuno.
11 Ikiwa
sisi tumepanda mbegu ya kiroho kati yenu, je, ni jambo kubwa tukichuma kwenu
faida ya kidunia?
12 Ikiwa
wengine wanayo haki ya kutazamia hayo kutoka kwenu, je, sisi hatuna haki zaidi
kuliko hao? Lakini, sisi hatukuitumia haki hiyo, Badala yake, tumestahimili
kila kitu ili tusiiwekee kizuizi chochote Habari Njema ya Kristo.
13 Je,
hamjui kwamba wanaotumikia Hekaluni hupata chakula chao Hekaluni, na kwamba
wanaotolea sadaka madhabahuni hupata sehemu ya hiyo sadaka?
14 Bwana
aliagiza vivyo hivyo; wahubiri wa Habari Njema wapate riziki zao kutokana nayo.
15 Lakini,
mimi sikutumia hata mojawapo ya haki hizo. Na wala siandiki nijipatie haki
hizo; kwangu mimi ni afadhali kufa kuliko kumfanya yeyote aone kwamba najisifu
bure.
16 Ikiwa
ninaihubiri Habari Njema, hilo si jambo la kujivunia; hilo ni jukumu
nililopewa. Na, ole wangu kama sitaihubiri Habari Njema!
17
Ningekuwa nimeichagua kazi hii kwa hiari, basi, ningetazamia malipo; lakini
maadam naifanya ikiwa ni wajibu, hiyo ina maana kwamba ni jukumu nililopewa
nitekeleze.
18
Mshahara wangu ni kitu gani, basi? Mshahara wangu ni fursa ya kuihubiri Habari
Njema bure, bila kudai haki ninazostahili kwa kuihubiri.
19 Kwa
hiyo, ingawa mimi si mtumwa wa mtu yeyote, nimejifanya mtumwa wa kila mtu ili
nimpatie Kristo watu wengi iwezekanavyo.
20 Kwa
Wayahudi nimeishi kama Myahudi ili niwapate Wayahudi; yaani, ingawa mimi siko
chini ya Sheria, nimejiweka chini ya Sheria kwao, ili niwapate hao walio chini
ya Sheria.
21 Na kwa
wale walio nje ya Sheria, naishi kama wao, nje ya Sheria, ili niwapate hao
walio nje ya Sheria. Hii haimaanishi kwamba mimi niko nje ya sheria ya Mungu,
maana nabanwa na sheria ya Kristo.
22 Kwao
walio dhaifu nimejifanya dhaifu ili niwapate hao walio dhaifu. Nimejifanya kila
kitu kwa wote ili nipate kuwaokoa baadhi yao kwa kila njia.
23 Nafanya
haya yote kwa ajili ya Habari Njema, nipate kushiriki baraka zake.
24 Je,
hamjui kwamba katika uwanja wa michezo, ingawa wapiga mbio wote hukimbia, ni
mmoja tu anayejinyakulia zawadi?
25
Wanariadha hujipa mazoezi na nidhamu kali; hufanya hivyo ili wajipatie taji
iharibikayo! Lakini sisi twafanya hivyo tupate taji ya kudumu daima.
26 Ndivyo
basi, ninavyopiga mbio nikiwa na nia ya kushinda; ndivyo ninavyopigana, na si
kama bondia anayetupa ngumi zake hewani.
27 Naupa
mwili wangu mazoezi magumu na kuutia katika nidhamu kamili, nisije mimi
mwenyewe nikakataliwa baada ya kuwahubiria wengine. ic
|