Chapter 2
1 Ninyi
mlikuwa mmekufa kwa sababu ya makosa na dhambi zenu.
2 Wakati
ule mliishi kufuatana na mtindo mbaya wa ulimwengu huu, mkawa mnamtii mtawala
wa pepo wenye nguvu wa anga, pepo ambao huwatawala sasa watu wasiomtii Mungu.
3 Na hata
sisi sote tulikuwa kama wao; tuliishi kufuatana na tamaa zetu za kidunia na
kufanya tu mambo yale yaliyoipendeza miili na akili zetu. Kidunia, sisi kama
vile pia wao, tulistahili ghadhabu ya Mungu.
4 Lakini
Mungu ni mwenye huruma nyingi. Alitupenda kwa mapendo yasiyopimika,
5 hata,
ingawa tulikuwa tumekufa kwa sababu ya dhambi, alitufanya hai pamoja na Kristo.
Kwa neema ya Mungu ninyi mmeokolewa.
6 Kwa
kuungana na Kristo Yesu, Mungu alitufufua pamoja naye, tukatawale pamoja naye
mbinguni.
7 Ndivyo
alivyopenda kuonyesha kwa watu wa nyakati za baadaye, ukuu wa neema yake
aliyotujalia kwa ukarimu katika kuungana kwetu na Kristo Yesu.
8 Maana,
kwa neema ya Mungu mmekombolewa kwa njia ya imani. Jambo hili si matokeo ya
juhudi zenu, bali ni zawadi ya Mungu.
9 Wala
halitokani na matendo yenu wenyewe, asije mtu akajivunia kitu.
10 Sisi ni
viumbe vyake Mungu, na kwa kuungana na Kristo Yesu, alituumba kwa ajili ya
kuishi maisha ya matendo mema aliyotutayarishia tuyatende.
11 Ninyi
mlio kwa asili watu wa mataifa mengine - mnaoitwa, "wasiotahiriwa" na
Wayahudi ambao hujiita, "Waliotahiriwa," (kwa sababu ya kile
wanachoifanyia miili yao) - kumbukeni mlivyokuwa zamani.
12 Wakati
ule ninyi mlikuwa bila Kristo; mlikuwa nje ya jamii ya Israeli; mlikuwa wageni
na hamkuwa na sehemu yoyote katika lile agano la zile ahadi. Mlikuwa bila
matumaini Mungu hapa duniani.
13 Lakini
sasa, kwa kuungana na Kristo Yesu, ninyi ambao hapo awali mlikuwa mbali,
mmekaribishwa kwa njia ya damu yake Kristo.
14 Maana
Kristo mwenyewe ametuletea amani kwa kuwafanya Wayahudi na watu wa mataifa
mengine kuwa jamii moja. Kwa mwili wake yeye mwenyewe aliubomoa ule ukuta
uliowatenganisha na kuwafanya maadui.
15 Aliiondoa
ile Sheria ya Wayahudi pamoja na amri zake na kanuni zake, ili kutokana na
jamii hizo mbili aumbe jamii moja mpya katika umoja naye na hivyo kuleta amani.
16 Kwa
mwili wake, Kristo aliuangamiza uadui wao; kwa msalaba wake aliziunganisha
jamii hizo kuwa moja na kuzipatanisha na Mungu.
17 Basi,
Kristo alikuja akahubiri Habari Njema ya amani kwenu ninyi watu wa mataifa
mengine mliokuwa mbali na Mungu, na pia kwa Wayahudi ambao walikuwa karibu na
Mungu.
18 Hivyo,
kwa njia yake, sisi sote, Wayahudi na watu wa mataifa mengine, tunaweza
kumwendea Baba katika Roho mmoja.
19 Basi,
ninyi si wageni tena, wala si watu wa nje; ninyi ni raia pamoja na watu wa
Mungu, na ni watu wa jamaa ya Mungu.
20
Mmejengwa juu ya msingi uliowekwa na mitume na manabii, naye Kristo mwenyewe
ndiye jiwe kuu la msingi.
21 Yeye
ndiye mwenye kulitengeneza jengo lote na kulikuza hata liwe hekalu takatifu kwa
ajili ya B wana.
22 Katika
kuungana naye, ninyi pia mnajengwa pamoja na wote wengine, muwe makao ya Mungu
kwa njia ya Roho wake.
|