Chapter 3
1 Mwishowe hatukuweza kuvumilia zaidi. Basi, tuliamua kubaki kule Athene peke yetu,
2 na
kumtuma kwenu ndugu yetu Timotheo, ambaye ni mfanyakazi mwenzetu kwa ajili ya
Mungu katika kuhubiri Habari Njema ya Kristo. Tulimtuma ili awaimarisheni na
kuwafarijini,
3 kusudi
imani ya mtu yeyote miongoni mwenu isije ikafifia kwa sababu ya taabu hizo.
Ninyi mnajua kwamba tunapaswa kupata mateso.
4 Maana,
tulipokuwa pamoja nanyi, tuliwaambieni kwamba tutateswa; na kama mjuavyo ndivyo
ilivyotukia.
5 Ndio
maana nilimtuma Timotheo kwenu. Sikuweza kungoja zaidi, na hivyo nilimtuma
nipate habari za imani yenu. Isije ikawa labda Mshawishi aliwajaribuni na kazi
yote tuliyofanya miongoni mwenu imepotea bure!
6 Sasa
Timotheo amekwisha rudi, naye ametupa habari za kufurahisha kuhusu imani na
upendo wenu. Ametuarifu kwamba mnatukumbuka daima, na kwamba mna hamu ya
kutuona sisi kama nasi tulivyo na hamu ya kuwaoneni.
7 Basi,
habari za imani yenu zimetutia moyo katika taabu na mateso yetu yote,
8 kwani
sasa tunaishi kweli ikiwa ninyi mnasimama imara katika kuungana na Bwana.
9 Sasa
twaweza kumshukuru Mungu wetu kwa ajili yenu. Tunamshukuru kwa furaha tuliyo
nayo mbele yake kwa sababu yenu.
10
Tunazidi kumwomba Mungu usiku na mchana kwa moyo wetu wote ili atupatie fursa
ya kuwaoneni uso kwa uso ili tuweze kurekebisha chochote kilichopungua katika
imani yenu.
11
Tunamwomba Mungu, Baba yetu mwenyewe, na Bwana wetu Yesu atutayarishie njia ya
kuja kwenu.
12 Bwana
awawezeshe ninyi kupendana na kuwapenda watu wote zaidi na zaidi, kama vile
sisi tunavyowapenda ninyi.
13 Hivyo
ataiimarisha mioyo yenu, nanyi mtakuwa wakamilifu na watakatifu mbele ya Mungu
na Baba yetu wakati Bwana wetu Yesu atakapokuja pamoja na wote walio wake.
1
Thessalonians
|