Chapter 4
1
Hatimaye, ndugu zangu, mmejifunza kutoka kwetu namna mnavyopaswa kuishi ili
kumpendeza Mungu. Na kweli mmekuwa mnaishi hivyo. Sasa tunawaombeni na kuwasihi
kwa jina la Bwana Yesu mfanye vema zaidi.
2 Maana
mnayajua yale maagizo tuliyowapeni kwa mamlaka ya Bwana Yesu.
3 Mungu
anataka ninyi muwe watakatifu na mjiepushe kabisa na maisha ya zinaa.
4 Kila
mwanamume anapaswa kujua namna ya kuishi na mkewe kwa utakatifu na heshima,
5 na si
kwa tamaa mbaya kama watu wa mataifa mengine wasiomjua Mungu.
6 Basi,
mtu yeyote asimkosee au kumpunja mwenzake kuhusu jambo hili. Tulikwisha
waambieni hayo na kuwaonya kwamba Bwana atawaadhibu wanaofanya mambo hayo.
7 Mungu
hakutuita tuishi maisha ya zinaa, bali tuishi katika utakatifu.
8 Kwa hiyo
basi, anayedharau mafundisho hayo hamdharau mtu, bali amdharau Mungu mwenyewe
anayewapeni Roho wake Mtakatifu.
9 Hakuna
haja ya kuwaandikieni juu ya kuwapenda ndugu zenu waumini. Ninyi wenyewe mmefundishwa
na Mungu namna mnavyopaswa kupendana.
10 Na
mmekuwa mkiwatendea hivyo ndugu zenu wote kila mahali katika Makedonia. Basi,
ndugu tunawaombeni mfanye hata zaidi.
11 Muwe na
nia ya kuishi maisha ya utulivu, kila mmoja ashughulikie mambo yake mwenyewe na
afanye kazi kwa mikono yake mwenyewe kama tulivyowaagiza pale awali.
12 Kwa
namna hiyo mtajipatia sifa nzuri kutoka kwa wale wasio Wakristo, na hamtakuwa
na lazima ya kuwategemea wengine kwa mahitaji yenu.
13 Ndugu,
twataka mjue ukweli kuhusu wale ambao wamekwisha fariki dunia, ili msipatwe na
huzuni kama watu wengine wasio na matumaini.
14 Sisi
tunaamini kwamba Yesu alikufa, akafufuka; na hivyo sisi tunaamini kwamba Mungu
atawaleta pamoja na Yesu wale wote waliofariki wakiwa wanamwamini.
15 Hili
tunalowaambieni ni fundisho la Bwana; sisi tulio hai, ambao tutakuwa tumebaki,
wakati Bwana atakapokuja, hakika hatutawatangulia wale waliokwisha fariki dunia.
16 Maana
patatolewa amri, sauti ya malaika mkuu, sauti ya tarumbeta ya Mungu, naye Bwana
mwenyewe atashuka kutoka mbinguni. Ndipo wale waliokufa wakiwa wanamwamini
Kristo watafufuliwa kwanza.
17 Kisha
sisi tulio hai wakati huo tutakusanywa pamoja nao katika mawingu kumlaki Bwana
hewani. Na hivyo tutakuwa daima pamoja na Bwana.
18 Basi,
farijianeni kwa maneno haya.
1
Thessalonians
|