Chapter 5
1 Ndugu,
hakuna haja ya kuwaandikieni juu ya nyakati na majira yatakapotukia mambo haya.
2 Maana
ninyi wenyewe mwajua kwamba Siku ya Bwana itakuja kama mwizi ajavyo usiku.
3 Watu
watakapokuwa wanasema: "Kila kitu ni shwari na salama" ndipo
uharibifu utakapowaangukia ghafla! Mambo hayo yatatukia ghafla kama uchungu wa uzazi unavyomjia mama
anayejifungua, wala watu hawataweza kuepukana nayo.
4 Lakini
ninyi ndugu, hamko gizani, na siku hiyo haipaswi kuwajieni ghafla kama vile mwizi.
5 Ninyi
nyote ni watu mnaoishi katika mwanga, watu wa mchana. Sisi si watu wa usiku,
wala wa giza.
6 Basi,
tusilale usingizi kama
wengine; tunapaswa kukesha na kuwa na kiasi.
7
Wanaolala hulala usiku, na walevi hulewa usiku.
8 Lakini
sisi ni watu wa mchana na tunapaswa kuwa na kiasi. Tunapaswa kuvaa imani na
upendo kama vazi la kujikinga kifuani, na
tumaini letu la wokovu kama
kofia ya chuma.
9 Maana
Mungu hakututeua ili tuangamizwe na ghadhabu yake, bali tuupate wokovu kwa njia
ya Bwana wetu Yesu Kristo,
10 ambaye
alikufa kwa ajili yetu, ili tuishi pamoja naye, iwe tu hai au tumekufa.
11 Kwa
hiyo farijianeni na kusaidiana ninyi kwa ninyi kama mnavyofanya sasa.
12 Ndugu,
tunawaombeni muwastahi wale wanaofanya kazi kati yenu, wale wanaowaongoza na
kuwafundisheni kuhusu maisha ya Kikristo.
13 Wapeni
heshima kubwa na kuwapenda kwa sababu ya kazi wanayofanya. Muwe na amani kati
yenu.
14 Ndugu,
tunawahimizeni muwaonye watu walio wavivu, muwatie moyo watu wanyonge,
muwasaidie watu dhaifu, muwe na subira kwa wote.
15
Angalieni mtu yeyote asimlipe mwingine maovu kwa maovu, ila nia yenu iwe
kutendeana mema daima na kuwatendea mema watu wote.
16 Furahini daima,
17 salini kila wakati
18 na muwe
na shukrani katika kila hali. Hayo ndiyo anayotaka Mungu kwenu katika kuungana
kwenu na Kristo Yesu.
19
Msimpinge Roho Mtakatifu;
20
msidharau unabii.
21 Pimeni
kila kitu: zingatieni kilicho chema,
22 na
epukeni kila aina ya uovu.
23 Mungu
anayetupatia amani awafanye ninyi watakatifu kwa kila namna na kuzilinda nafsi
zenu - roho, mioyo na miili yenu - mbali na hatia yoyote wakati wa kuja kwake
Bwana wetu Yesu Kristo.
24 Yeye
anayewaita ninyi atafanya hivyo kwani ni mwaminifu.
25 Ndugu, tuombeeni na sisi pia.
26 Wasalimuni ndugu wote kwa ishara ya upendo.
27 Nawahimizeni kwa jina la Bwana muwasomee ndugu zetu wote
barua hii.
28 Tunawatakieni neema ya Bwana wetu Yesu Kristo.
Chapter 2
|