2 Thessalonians
Chapter 1
1 Mimi
Paulo, Silwano na Timotheo tunawaandikia ninyi jumuiya ya kanisa la
Thesalonike, ambao ni watu wake Mungu Baba yetu na wa Bwana Yesu Kristo.
2
Tunawatakieni neema na amani kutoka kwa Mungu Baba yetu na kwa Bwana Yesu
Kristo.
3 Ndugu,
tunapaswa kushukuru Mungu daima kwa ajili yenu. Inafaa kwetu kufanya hivyo
kwani imani yenu inakua sana na kupendana kwenu kunaongezeka sana.
4 Ndio
maana sisi tunajivunia ninyi katika makanisa ya Mungu. Tunaona fahari juu ya
jinsi mnavyoendelea kuamini na kustahimili katika udhalimu wote na mateso
mnayopata.
5 Hayo
yote yanathibitisha kwamba hukumu ya Mungu ni ya haki, na matokeo yake ninyi
mtastahili Utawala wake ambao kwa ajili yake mnateseka.
6 Mungu
atafanya jambo la haki: atawalipa mateso wale wanaowatesa ninyi,
7 na
kuwapeni nafuu ninyi mnaoteseka, na sisi pia. Atafanya jambo hilo wakati Bwana
atakapotokea kutoka mbinguni pamoja na malaika wake na wakuu
8 na miali
ya moto, kuwaadhibu wale wanaomkataa Mungu na wale wasiotii Habari Njema ya
Bwana wetu Yesu.
9 Adhabu
yao itakuwa kuangamizwa milele na kutengwa mbali na utukufu wake mkuu,
10 wakati
atakapokuja Siku ile kupokea utukufu kutoka kwa watu wake na heshima kutoka kwa
wote wanaoamini. Ninyi pia mtakuwa miongoni mwao, kwani mmeuamini ule ujumbe
tuliowaletea.
11 Ndiyo maana tunawaombeeni daima. Tunamwomba Mungu wetu
awawezeshe muyastahili maisha aliyowaitia myaishi. Tunamwomba, kwa uwezo wake,
atimize nia yenu ya kutenda mema na kukamilisha kazi yenu ya imani.
12 Kwa namna hiyo, jina la Bwana wetu Yesu litapata utukufu
kutoka kwenu, nanyi mtapata utukufu kutoka kwake kwa neema ya Mungu wetu na ya
Bwana Yesu Kristo.
2 Thessalonians
|