Chapter 3
1 Hatimaye, ndugu, tuombeeni ili ujumbe wa Bwana uzidi kuenea
upesi na kupokelewa kwa heshima kama vile ulivyo kati yenu.
2 Ombeni pia ili Mungu atuokoe na watu wapotovu na waovu,
maana si wote wanaoamini ujumbe huu.
3 Lakini Bwana ni mwaminifu. Yeye atawaimarisheni na kuwalinda salama na
yule Mwovu.
4 Naye
Bwana anatupatia tumaini kubwa juu yenu, na hatuna shaka kwamba mnafanya na
mtaendelea kufanya yale tuliyowaambieni.
5 Bwana aiongoze
mioyo yenu katika upendo wa Mungu na katika uvumilivu tunaopewa na Kristo.
6 Ndugu,
tunawaamuru kwa jina la Bwana wetu Yesu Kristo, mjiepushe na ndugu wote walio
wavivu na ambao hawafuati maagizo tuliyowapa.
7 Ninyi
wenyewe mnajua kwamba mnapaswa kufuata mfano wetu. Sisi tulipokuwa nanyi
hatukuwa wavivu;
8 hatukula
chakula kwa mtu yeyote bila ya kumlipa. Tulifanya kazi kwa bidii na taabu
mchana na usiku ili tusiwe mzigo kwa mtu yeyote kati yenu.
9
Tulifanya hivyo si kwa kuwa hatuna haki ya kutaka msaada wenu, ila kwa sababu
tunataka kuwapeni mfano.
10
Tulipokuwa pamoja nanyi tulikuwa tukiwaambieni, "Mtu asiyefanya kazi,
asile."
11
Tunasema mambo hayo kwa sababu tumesikia kwamba wako baadhi yenu ambao ni
wavivu na ambao hawafanyi chochote, isipokuwa tu kujiingiza katika mambo ya
watu wengine.
12 Kwa
jina la Bwana wetu Yesu Kristo tunawaamuru na kuwaonya watu hao wawe na nidhamu
na kufanya kazi ili wajipatie maslahi yao wenyewe.
13 Lakini
ninyi ndugu, msichoke kutenda mema.
14 Huenda
kwamba huko kuna mtu ambaye hatautii huu ujumbe tunaowapelekeeni katika barua
hii. Ikiwa hivyo, basi, mfichueni mtu huyo na msiwe na uhusiano wowote naye
kusudi aone aibu.
15 Lakini
msimtendee mtu huyo kama adui, bali mwonyeni kama ndugu.
16 Bwana
mwenyewe ndiye chanzo cha amani, awajalieni amani siku zote kwa kila namna.
Bwana awe nanyi nyote.
17 Kwa
mkono wangu mwenyewe naandika hivi: Salamu kutoka kwa Paulo! Hivi ndivyo
ninavyotia sahihi kila barua; ndivyo ninavyoandika.
18
Tunawatakieni nyote neema ya Bwana wetu Yesu Kristo.
|