Chapter 5
1
Usimkemee mtu mzee, bali msihi kama vile angekuwa baba yako. Watendee vijana
kama ndugu zako,
2 wanawake
wazee kama mama yako, na wasichana kama dada zako, kwa usafi wote.
3
Waheshimu wanawake wajane walio wajane kweli.
4 Lakini
mjane aliye na watoto au wajukuu, hao wanapaswa kujifunza kutimiza wajibu wao
wa kidini kwa jamaa zao wenyewe na hivyo kuwalipa wazazi wao na wazee wao,
kwani hilo ni jambo la kupendeza mbele ya Mungu.
5 Mwanamke
mjane kweli, asiye na mtu wa kumsaidia, amemwekea Mungu tumaini lake na
huendelea kusali na kumwomba msaada usiku na mchana.
6 Lakini
mwanamke ambaye huishi maisha ya anasa, huyo amekufa, ingawa yu hai.
7 Wape
maagizo haya, wasije wakawa na lawama.
8 Lakini
kama mtu hawatunzi watu wa jamaa yake, hasa wale wa nyumbani kwake, basi, mtu
huyo ameikana imani, na ni mbaya zaidi kuliko mtu asiyeamini.
9 Usimtie katika
orodha ya wajane, mjane yeyote ambaye hajatimiza miaka sitini. Tena awe amepata
kuolewa mara moja tu,
10 na awe
mwenye sifa nzuri: aliyewalea watoto wake vizuri, aliyewakaribisha wageni
nyumbani kwake, aliyewaosha miguu watu wa Mungu, aliyewasaidia watu wenye
taabu, na aliyejitolea kufanya mambo mema.
11
Usiwaandikishe wajane vijana, kwani kama tamaa zao za maumbile zikizidi kuwa na
nguvu zaidi kuliko kujitolea kwao kwa Kristo watataka kuolewa tena,
12 na
wataonekana kukosa uaminifu kuhusu ahadi yao ya pale awali.
13 Wajane
kama hao huanza kupoteza wakati wao wakizurura nyumba hata nyumba; tena ubaya
zaidi ni kwamba huanza kuwasengenya watu, na kujitia katika mambo ya watu
wengine, huku wakisema mambo ambayo hawangepaswa kusema.
14 Kwa
hiyo ningependelea wajane vijana waolewe, wapate watoto na kutunza nyumba zao
ili adui zetu wasipewe nafasi ya kusema mambo maovu juu yetu.
15 Kwa
maana wajane wengine wamekwisha potoka na kumfuata Shetani.
16 Lakini
kama mama Mkristo anao wajane katika jamaa yake, yeye anapaswa kuwatunza na si
kuliachilia kanisa mzigo huo, ili kanisa liweze kuwatunza wajane wale waliobaki
peke yao kabisa.
17 Wazee
wanaowaongoza watu vizuri wanastahili kupata riziki maradufu, hasa wale
wanaofanya bidii katika kuhubiri na kufundisha.
18 Maana
Maandiko Matakatifu yasema: "Usimfunge ng`ombe kinywa anapopura
nafaka." na tena "Mfanyakazi astahili malipo yake."
19
Usikubali kupokea mashtaka dhidi ya mzee yasipowakilishwa na mashahidi wawili
au watatu.
20 Wale
wanaotenda dhambi waonye hadharani, ili wengine wapate kuogopa.
21
Nakuamuru mbele ya Mungu, mbele ya Kristo Yesu, na mbele ya malaika watakatifu
uyazingatie maagizo haya bila kuacha hata moja, wala kumpendelea mtu yeyote
katika kila unachotenda.
22
Usiharakishe kumwekea mtu yeyote mikono kwa ajili ya kumtumikia Bwana. Usishiriki
dhambi za wengine; jiweke katika hali safi.
23 Usinywe
maji tu, bali unywe divai kidogo kwa ajili ya tumbo lako, kwani unaugua mara
kwa mara.
24 Dhambi
za watu wengine huonekana waziwazi, nazo zawatangulia kwenye hukumu; lakini
dhambi za wengine huonekana tu baadaye.
25 Vivyo
hivyo, matendo mema huonekana waziwazi, na hata yale ambayo si dhahiri hayawezi
kufichika.
|