Chapter 4
1
Nakuamuru mbele ya Mungu, na mbele ya Kristo Yesu atakayewahukumu watu walio
hai na wafu, na kwa sababu anakuja kutawala akiwa Mfalme:
2 hubiri
huo ujumbe, sisitiza kuutangaza (iwe ni wakati wa kufaa au wakati usiofaa),
karipia, onya na himiza watu ukiwafundisha kwa uvumilivu wote.
3 Utakuja
wakati ambapo watu hawatasikiliza mafundisho ya kweli, ila watafuata tamaa zao
wenyewe na kujikusanyia walimu tele watakaowaambia mambo yale tu ambayo masikio
yao yako tayari kusikia.
4
Watakataa kuusikia ukweli, watageukia hadithi za uongo.
5 Wewe,
lakini, uwe macho katika kila hali; vumilia mateso, fanya kazi ya mhubiri wa
Habari Njema, timiza kikamilifu utumishi wako.
6 Kwa
upande wangu mimi, niko karibu kabisa kutolewa dhabihu na wakati wa kufariki
kwangu umefika.
7
Nimefanya bidii katika mashindano, nimemaliza safari yote na imani nimeitunza.
8 Na sasa
imebakia tu kupewa tuzo la ushindi kwa maisha ya uadilifu, tuzo ambalo Bwana
Hakimu wa haki, atanipa mimi Siku ile na wala si mimi tu, ila na wale wote
wanaotazamia kwa upendo kutokea kwake.
9 Fanya
bidii kuja kwangu karibuni.
10 Dema
ameupenda ulimwengu huu akaniacha na kwenda zake Thesalonike. Kreske amekwenda
Galatia, na Tito amekwenda Dalmatia.
11 Luka
peke yake ndiye aliye hapa pamoja nami. Mpate Marko uje naye, kwa maana ataweza
kunisaidia katika kazi yangu.
12
Nilimtuma Tukiko kule Efeso.
13
Utakapokuja niletee koti langu nililoacha kwa Karpo kule Troa; niletee pia vile
vitabu, na hasa vile vilivyotengenezwa kwa ngozi. ic
14 Yule sonara
aitwaye Aleksanda amenitendea maovu mengi; Bwana atamlipa kufuatana na hayo
matendo yake.
15
Jihadhari naye kwa sababu aliupinga ujumbe wetu kwa ukali.
16 Wakati
nilipojitetea kwa mara ya kwanza hakuna mtu aliyesimama upande wangu; wote
waliniacha. Mungu asiwahesabie kosa hilo!
17 Lakini,
Bwana alikaa pamoja nami, akanipa nguvu, hata nikaweza kuutangaza ujumbe wote,
watu wa mataifa wausikie; tena nikaokolewa katika hukumu ya kifo kama kinywani
mwa simba.
18 Bwana
ataniokoa na mambo yote maovu, na kunichukua salama mpaka katika Utawala wake
wa mbinguni. Kwake uwe utukufu milele na milele! Amina.
19
Wasalimu Priska na Akula, pamoja na jamaa ya Onesiforo.
20 Erasto
alibaki Korintho, naye Trofimo nilimwacha Mileto kwa sababu alikuwa mgonjwa.
21 Fanya
bidii kuja kabla ya majira ya baridi. Ebulo, Pude, Lino na Klaudia
wanakusalimu; vilevile ndugu wengine wote.
22 Bwana
awe nawe rohoni mwako. Nawatakieni nyote neema.
|