Titus
Chapter 1
1 Mimi
Paulo, mtumishi wa Mungu na mtume wa Yesu Kristo naandika. Mimi nimechaguliwa
kuijenga imani ya wateule wa Mungu na kuwaongoza waufahamu ukweli wa dini yetu,
2 ambayo
msingi wake ni tumaini la kupata uzima wa milele. Mungu ambaye hasemi uongo,
alituahidia uzima huo kabla ya mwanzo wa nyakati,
3 na
wakati ufaao ulipowadia, akaudhihirisha katika ujumbe wake. Mimi nilikabidhiwa
ujumbe huo nuutangaze kufuatana na amri ya Mungu, Mwokozi wetu.
4
Ninakuandikia wewe Tito, mwanangu wa kweli katika imani tunayoshiriki.
Nakutakia neema na amani kutoka kwa Mungu Baba, na kutoka kwa Kristo Yesu,
Mkombozi wetu.
5
Nilikuacha Krete ili urekebishe yale mambo ambayo hayakuwa yamekamilika bado,
na kuwateua wazee wa kanisa katika kila mji. Kumbuka maagizo yangu:
6 mzee wa
kanisa anapaswa kuwa mtu asiye na hatia; aliye na mke mmoja tu, na watoto wake
wanapaswa kuwa waumini, wasiojulikana kuwa wakorofi au wakaidi.
7 Maana
kwa vile kiongozi wa kanisa ni mkurugenzi wa kazi ya Mungu, anapaswa kuwa mtu
asiye na hatia. Asiwe mwenye majivuno, mwepesi wa hasira, mlevi, mkorofi au
mchoyo.
8 Anapaswa
kuwa mkarimu na anayependa mambo mema. Anapaswa kuwa mtu mtaratibu, mwadilifu,
mtakatifu na mwenye nidhamu.
9 Ni
lazima ashike kikamilifu ujumbe ule wa kuaminika kama unavyofundishwa. Ndivyo
atakavyoweza kuwatia wengine moyo kwa mafundisho ya kweli na kuyafichua makosa
ya wale wanaoyapinga mafundisho hayo.
10 Maana,
wako watu wengi, hasa wale walioongoka kutoka dini ya Kiyahudi, ambao ni
wakaidi, wanaowapotosha wengine kwa upumbavu wao.
11 Lazima
kukomesha maneno yao, kwani wanavuruga jumuiya nzima kwa kufundisha mambo
ambayo hawapaswi kufundisha; wanafanya hivyo kwa nia mbaya ya kupata faida ya
fedha.
12 Hata
mmoja wa manabii wao, ambaye naye pia ni Mkrete, alisema: "Wakrete, husema
uongo daima; ni kama wanyama wabaya, walafi na wavivu!"
13 Naye
alitoboa ukweli kwa sababu hiyo, unapaswa kuwakaripia vikali, ili wawe na imani
kamilifu.
14
Wasiendelee kushikilia hadithi tupu za Kiyahudi na maagizo ya kibinadamu
yanayozuka kwa watu walioukataa ukweli.
15 Kila
kitu ni safi kwa watu walio safi; lakini hakuna chochote kilicho safi kwa wale
waliochafuliwa na wasioamini, maana dhamiri na akili zao zimechafuliwa.
16 Watu
kama hao hujidai kwamba wanamjua Mungu, lakini kwa matendo yao humkana. Ni watu
wa kuchukiza mno na wakaidi, hawafai kwa jambo lolote jema.
|