Philemon
Chapter 1
1 Mimi Paulo,
mfungwa kwa ajili ya Kristo Yesu, na ndugu Timotheo, ninakuandikia wewe
Filemoni mpendwa, mfanyakazi mwenzetu
2 na kanisa
linalokutana nyumbani kwako, na wewe dada Afia, na askari mwenzetu Arkupo.
3 Tunawatakieni
neema na amani kutoka kwa Mungu Baba yetu, na kwa Bwana yesu Kristo.
4 Kila wakati
ninaposali nakukumbuka wewe Filemoni, na kumshukuru Mungu
5 maana nasikia
habari za imani yako kwa Bwana wetu Yesu na upendo wako kwa watu wote wa Mungu.
6 Naomba ili
imani hiyo unayoshiriki pamoja nasi ikuwezeshe kuwa na ujuzi mkamilifu zaidi wa
baraka zote tunazopata katika kuungana kwetu na Kristo.
7 Ndugu, upendo
wako yameniletea furaha kubwa na kunipa moyo sana! Nawe umeichangamsha mioyo ya
watu wa Mungu.
8 Kwa sababu
hiyo, ningeweza, kwa uhodari kabisa, nikiwa ndugu yako katika Kristo, kukuamuru
ufanye unachopaswa kufanya.
9 Lakini kwa
sababu ya upendo, ni afadhali zaidi nikuombe. Nafanya hivi ingawa mimi ni
Paulo, balozi wa Kristo Yesu, na sasa pia mfungwa kwa ajili yake.
10 Basi, ninalo
ombi moja kwako kuhusu mwanangu Onesimo, ambaye ni mwanangu katika Kristo kwani
nimekuwa baba yake nikiwa kifungoni.
11 Ni Onesimo
yuleyule ambaye wakati mmoja alikuwa hakufai kitu, lakini sasa ananifaa mimi na
wewe pia.
12 Sasa
namrudisha kwako, naye ni kama moyo wangu mimi mwenyewe.
13 Ningependa
akae nami hapa anisaidie badala yako wakati niwapo kifungoni kwa sababu ya
Habari Njema.
14 Lakini sitafanya chochote bila kibali chako. Sipendi
kukulazimisha unisaidie, kwani wema wako unapaswa kutokana na hiari yako wewe
mwenyewe na si kwa kulazimika.
15 Labda Onesimo aliondoka kwako kwa kitambo tu, kusudi
uweze tena kuwa naye daima.
16 Na sasa yeye si mtumwa tu, ila ni bora zaidi ya mtumwa:
yeye ni ndugu yetu mpenzi. Na wa maana sana kwangu mimi, na kwako atakuwa wa
maana zaidi kama mtumwa na kama ndugu katika Bwana.
17 Basi, ikiwa wanitambua mimi kuwa mwenzako, mpokee tena
kama vile ungenipokea mimi mwenyewe.
18 Kama alikuwa amekukosea kitu, au alikuwa na deni lako,
basi, unidai mimi.
19 Naandika jambo hili kwa mkono wangu mwenyewe: yako.)
20 Haya, basi, ndugu yangu, nifanyie jambo hilo kwa ajili
ya jina la Bwana; burudisha moyo wangu kama ndugu katika Kristo.
21 Naandika nikitumaini kwamba utanikubalia ombi langu;
tena najua kwamba utafanya hata zaidi ya haya ninayokuomba.
22 Pamoja na hayo, nitayarishie chumba kwani natumaini
kwamba kwa sala zenu, Mungu atanijalia niwatembeleeni.
23 Epafra, mfungwa mwenzangu kwa ajili ya Kristo Yesu,
anakusalimu.
24 Nao akina Marko, Aristarko, Dema na Luka, wafanyakazi
wenzangu, wanakusalimu.
25 Nawatakieni ninyi nyote neema ya Bwana wetu Yesu Kristo.
|