Chapter 3
1 Ndugu
zangu watu wa Mungu ambao mmeitwa na Mungu, fikirini juu ya Yesu ambaye Mungu
alimtuma awe Kuhani Mkuu wa imani tunayoiungama.
2 Yeye
alikuwa mwaminifu kwa Mungu aliyemteua kufanya kazi yake kama vile Mose
alivyokuwa mwaminifu katika nyumba yote ya Mungu.
3 Mjenzi
wa nyumba hupata heshima zaidi kuliko hiyo nyumba yenyewe. Hali kadhalika naye
Yesu anastahili heshima kubwa zaidi kuliko Mose.
4 Kila
nyumba hujengwa na mjenzi fulani - na Mungu ndiye mjenzi wa vitu vyote.
5 Mose
alikuwa mwaminifu katika nyumba yote ya Bwana kama mtumishi, na alinena juu ya
mambo ambayo Mungu atayasema hapo baadaye.
6 Lakini
Kristo ni mwaminifu kama Mwana mwenye mamlaka juu ya nyumba ya Mungu. Sisi ni nyumba
yake kama tukizingatia uhodari wetu na uthabiti wetu katika kile
tunachotumainia.
7 Kwa
hiyo, basi, kama asemavyo Roho Mtakatifu: "Kama mkisikia sauti ya Mungu
leo,
8
msiifanye mioyo yenu kuwa migumu kama wazee wenu walivyokuwa wakati walipomwasi
Mungu; kama walivyokuwa siku ile kule jangwani,
9 Huko
wazee wenu walinijaribu na kunichunguza, asema Bwana, ingawa walikuwa wameyaona
matendo yangu kwa miaka arobaini.
10 Kwa
sababu hiyo niliwakasirikia watu hao nikasema, `Fikira za watu hawa zimepotoka,
hawajapata kamwe kuzijua njia zangu.`
11 Basi,
nilikasirika, nikaapa: `Hawataingia huko ambako ningewapa pumziko."`
12 Basi
ndugu, jihadharini asije akawako yeyote miongoni mwenu aliye na moyo mbaya
hivyo na asiyeamini hata kujitenga na Mungu aliye hai.
13 Maadamu
hiyo "Leo" inayosemwa katika Maandiko bado inatuhusu sisi, mnapaswa
kusaidiana daima, ili mtu yeyote miongoni mwenu asidanganywe na dhambi na kuwa
mkaidi.
14 Maana
sisi tunashirikiana na Kristo ikiwa tutazingatia kwa uthabiti tumaini
tulilokuwa nalo mwanzoni.
15
Maandiko yasema hivi: "Kama mkisikia sauti ya Mungu leo, msiifanye mioyo
yenu kuwa migumu kama wazee wenu walivyokuwa wakati walipomwasi Mungu."
16 Ni
akina nani basi, waliosikia sauti ya Mungu wakamwasi? Ni wale wote walioongozwa
na Mose kutoka Misri.
17 Mungu
aliwakasirikia akina nani kwa miaka arobaini? Aliwakasirikia wale waliotenda
dhambi, maiti zao zikatapakaa kule jangwani.
18 Mungu
alipoapa: "Hawataingia huko ambako ningewapa pumziko," alikuwa
anawasema akina nani? Alikuwa anasema juu ya hao walioasi.
19 Basi,
twaona kwamba hawakuingia huko kwa sababu hawakuamini.
|