Chapter 6
1 Basi,
tusonge mbele kwa yale yaliyokomaa na kuyaacha nyuma yale mafundisho ya mwanzo
ya Kikristo. Hatuhitaji kuweka msingi tena kwa kurudia yale mafundisho ya
mwanzo kama vile kuachana na matendo ya kifo, kumwamini Mungu;
2
mafundisho juu ya ubatizo na kuwekewa mikono; ufufuo wa wafu na hukumu ya
milele.
3 tusonge
mbele! Hayo tutayafanya, Mungu akitujalia.
4 Maana
watu wanaoiasi imani yao inawezekanaje kuwarudisha watubu tena? Watu hao
walikwisha kuwa katika mwanga wa Mungu, walikwisha onja zawadi ya mbinguni na
kushirikishwa Roho Mtakatifu;
5
walikwisha onja wema wa neno la Mungu na nguvu za ulimwengu ujao,
6 kisha wakaiasi imani yao! Haiwezekani kuwarudisha watubu
tena, kwa sababu wanamsulubisha tena Mwana wa Mungu na kumwaibisha hadharani.
7 Mungu huibariki ardhi ambayo huipokea mvua inayoinyeshea
mara kwa mara, na kuotesha mimea ya faida kwa mkulima.
8 Lakini kama ardhi hiyo ikiota miti ya miiba na magugu,
haina faida; karibu italaaniwa na Mungu na mwisho wake ni kuchomwa moto.
9 Lakini, ingawa twasema namna hii, wapenzi wetu, tunalo
tumaini kubwa juu ya hali yenu. Tunajua kwamba mmepokea baraka zile bora za
wokovu wenu.
10 Mungu hakosi haki; yeye hataisahau kazi mliyoifanya au
upendo mlioonyesha kwa ajili ya jina lake katika huduma mliyowapa na mnayowapa
sasa watu wake.
11 Hamu yetu ni kwamba kila mmoja wenu aonyeshe bidii
hiyohiyo mpaka mwisho, ili yale mnayotumainia yapate kutimia.
12 Msiwe wavivu, bali muwe kama wale wanaoamini na wenye
uvumilivu na hivyo wanapokea yake aliyoahidi Mungu.
13 Mungu alipompa Abrahamu ahadi, aliapa kwa jina lake
mwenyewe, maana hakuna aliye mkuu kuliko Mungu ambaye kwa huyo angeweza kuapa.
14 Mungu alisema: "Hakika nitakubariki na nitakupa
wazawa wengi."
15 Abrahamu alisubiri kwa uvumilivu na hivyo alipokea kile
alichoahidiwa na Mungu.
16 Watu wanapoapa, huapa kwa mmoja aliye mkuu zaidi kuliko
wao, na kiapo hicho husuluhisha ubishi wote.
17 Naye Mungu aliimarisha ahadi yake kwa kiapo; na kwa
namna hiyo akawaonyesha wazi wale aliowaahidia kwamba hatabadili nia yake.
18 Basi, kuna vitu hivi viwili: ahadi na kiapo, ambavyo
haviwezi kubadilika na wala juu ya hivyo Mungu hawezi kusema uongo. Kwa hiyo
sisi tuliokimbilia usalama kwake, tunapewa moyo wa kushikilia imara tumaini
lililowekwa mbele yetu.
19 Tunalo tumaini hilo kama nanga ya maisha yetu. Tumaini
hilo ni imara na thabiti, nalo lapenya lile pazia la hekalu la mbinguni mpaka
patakatifu ndani.
20 Yesu ametangulia kuingia humo kwa niaba yetu, na amekuwa
kuhani mkuu milele, kufuatana na utaratibu wa ukuhani wa Melkisedeki.
|