Chapter 6
1 "Jihadharini
msije mkafanya matendo yenu mema mbele ya watu kusudi mwonekane nao. La sivyo,
Baba yenu aliye mbinguni hatawapeni tuzo.
2
"Basi, unapomsaidia maskini, usijitangaze. Usifanye kama wanafiki
wafanyavyo katika masunagogi na njiani ili watu wawasifu. Kweli nawaambieni,
hao wamekwisha pata tuzo lao.
3 Lakini
wewe unapomsaidia maskini, fanya hivyo kwamba hata rafiki yako asijue ufanyalo.
4 Toa
msaada wako kwa siri, na Baba yako aonaye yaliyofichika, atakutuza.
5
"Mnaposali, msifanye kama wanafiki. Wao hupenda kusimama na kusali katika
masunagogi na katika pembe za njia ili watu wawaone. Kweli nawaambieni, hao
wamekwisha pata tuzo lao.
6 Lakini
wewe unaposali, ingia chumbani mwako, funga mlango, kisha umwombe Baba yako
asiyeonekana. Naye Baba yako aonaye yaliyofichika, atakutuza.
7
"Mnaposali, msipayuke maneno kama watu wasiomjua Mungu. Wao hudhani kwamba
Mungu atawasikiliza ati kwa sababu ya maneno mengi.
8 Msiwe
kama wao. Baba yenu anajua mnayoyahitaji hata kabla ya kumwomba.
9 Basi,
hivi ndivyo mnavyopaswa kusali: `Baba yetu uliye mbinguni: Jina lako litukuzwe.
10 Ufalme
wako ufike. Utakalo lifanyike duniani kama mbinguni.
11 Utupe leo chakula chetu tunachohitaji.
12 Utusamehe makosa yetu, kama nasi tunavyowasamehe
waliotukosea.
13 Usitutie katika majaribu, lakini utuokoe na yule Mwovu.`*fa*
na utukufu, hata milele. Amina.
14 "Maana mkiwasamehe watu makosa yao, Baba yenu wa
mbinguni atawasamehe ninyi pia.
15 Lakini msipowasamehe watu makosa yao, naye Baba yenu
hatawasamehe ninyi makosa yenu.
16 "Mnapofunga, msiwe na huzuni kama wanafiki. Wao
hukunja nyuso zao wapate kuonekana na watu kuwa wanafunga. Nawaambieni hakika,
hao wamekwisha pata tuzo lao.
17 Wewe lakini unapofunga, paka kichwa chako mafuta, nawa
uso wako,
18 ili mtu yeyote asijue kwamba unafunga, ila ujulikane tu
kwa Baba yako asiyeonekana. Naye Baba yako aonaye yaliyofichika atakutuza.
19 "Msijiwekee hazina hapa duniani ambako nondo na
kutu huharibu, na wezi huingia na kuiba.
20 Jiwekeeni hazina mbinguni ambako nondo na kutu hawawezi
kuiharibu, wala wezi hawaingii wakaiba.
21 Maana pale ilipo hazina yako, ndipo pia utakapokuwa moyo
wako.
22 "Jicho ni taa ya mwili. Kama jicho lako ni zima,
mwili wako wote utakuwa katika mwanga.
23 Lakini ikiwa jicho lako ni bovu, mwili wako wote utakuwa
katika giza. Basi, ikiwa mwanga ulioko ndani yako ni giza, basi, hilo ni giza
la kutisha mno.
24 "Hakuna mtu awezaye kutumikia mabwana wawili. Maana
atamchukia mmoja na kumpenda huyo wa pili; au ataambatana na mmoja na kumdharau
huyo mwingine. Hamwezi kumtumikia Mungu na mali pamoja.
25 "Ndiyo maana nawaambieni, msiwe na wasiwasi juu ya
chakula na kinywaji mnavyohitaji ili kuishi, wala juu ya mavazi mnayohitaji kwa
ajili ya miili yenu. Je, maisha ni
chakula tu au zaidi? Na mwili, je, si zaidi ya mavazi?
26 Waangalieni
ndege wa mwituni: hawapandi, hawavuni, wala hawana ghala yoyoye. Hata hivyo,
Baba yenu wa mbinguni huwalisha. Je, ninyi si wa thamani kuliko hao?
27 Ni nani
miongoni mwenu kwa kuwa na wasiwasi sana anaweza kuuongeza muda wa maisha yake?
28 "Na
kuhusu mavazi, ya nini kuwa na wasiwasi? Tazameni maua ya porini jinsi
yanavyostawi. Hayafanyi kazi wala hayasokoti.
29 Lakini
nawaambieni, hata Solomoni mwenyewe na fahari zake zote hakupata kuvikwa vizuri
kama ua mojawapo.
30 Ikiwa basi
Mungu hulivika hivyo jani la shambani ambalo leo liko na kesho latupwa motoni,
je, hatafanya zaidi kwenu ninyi? Enyi watu wenye imani haba!
31 "Basi,
msiwe na wasiwasi: `Tutakula nini, tutakunywa nini, tutavaa nini!`
32 Maana hayo
yote yanahangaikiwa na watu wasiomjua Mungu. Baba yenu wa mbinguni anajua
kwamba mnahitaji vitu hivyo vyote.
33 Bali,
zingatieni kwanza Ufalme wa Mungu na matakwa yake, na hayo mengine yote mtapewa
kwa ziada.
34 Basi, msiwe
na wasiwasi juu ya kesho; kesho inayo yake. Matatizo ya siku moja yanawatosheni
kwa siku hiyo.
|