Chapter 5
1 wazee! Mimi
niliye mzee ninalo ombi moja kwenu wazee wenzangu. Mimi mwenyewe nilishuhudia
kwa macho yangu mateso ya Kristo na natumaini kuushiriki ule utukufu
utakaofunuliwa. Mimi nawaombeni
2
mlichunge lile kundi la Mungu mlilokabidhiwa, mlitunze si kwa kulazimika, bali
kwa hiari kama atakavyo Mungu. Fanyeni kazi hiyo si kwa tamaa ya fedha, bali
kwa moyo wenu wote.
3
Msiwatawale kwa mabavu hao waliowekwa chini ya ulinzi wenu, bali muwe mfano kwa
hilo kundi.
4 Na wakati
Mchungaji Mkuu atakapotokea, ninyi mtapokea taji ya utukufu isiyofifia.
5
Kadhalika nanyi vijana mnapaswa kujiweka chini ya mamlaka ya wazee. Ninyi nyote
mnapaswa kuwa na unyenyekevu mpate kutumikiana; maana Maandiko Matakatifu yasema:
"Mungu huwapinga wenye majivuno, lakini huwajalia neema
wanyenyekevu."
6 Basi,
nyenyekeeni chini ya mkono wa enzi wa Mungu, ili awainue wakati ufaao.
7 Mwekeeni
matatizo yenu yote, maana yeye anawatunzeni.
8 Muwe
macho; kesheni! Maana adui yenu, Ibilisi, huzungukazunguka kama simba
angurumaye akitafuta mawindo.
9 Muwe
imara katika imani na kumpinga, mkijua kwamba ndugu zenu pote duniani wanapatwa
na mateso hayohayo.
10 Lakini
mkisha teseka muda mfupi, Mungu aliye asili ya neema yote na ambaye anawaiteni
muushiriki utukufu wake wa milele katika kuungana na Kristo, yeye mwenyewe
atawakamilisheni na kuwapeni uthabiti, nguvu na msingi imara.
11 Kwake
uwe uwezo milele! Amina.
12
Nimewaandikieni barua hii fupi kwa msaada wa Silwano, ndugu ambaye namjua na
kumwamini. Nataka kuwapeni moyo na kushuhudia kwamba jambo hili ni neema ya
Mungu kweli. Kaeni imara katika neema hiyo.
13 Jumuiya
ya wenzenu walioteuliwa na Mungu hapa Babuloni wanawasalimuni. Vilevile
mwanangu Marko anawasalimuni.
14
Salimianeni kwa ishara ya upendo wa Kikristo. Nawatakieni amani ninyi mlio wake
Kristo.
|