1 John
Chapter 1
1 Habari
hii ya yahusu Neno la uzima lililokuwako tangu mwanzo. Sisi tumepata kulisikia
na kuliona kwa macho yetu wenyewe; tulilitazama na kulishika kwa mikono yetu
wenyewe.
2 Uzima
huo ulipotokea sisi tuliuona na sasa tunasema habari zake na kuwaambieni juu ya
uzima huo wa milele uliokuwa kwa Baba na uliodhihirishwa kwetu.
3
Tulichokiona na kukisikia ndicho tunachowatangazieni ninyi pia ili nanyi mpate
kushirikiana nasi katika umoja tulio nao na Baba na Mwanae Yesu Kristo.
4
Tunawaandikia ninyi mambo haya kusudi furaha yetu ikamilike.
5 Basi,
habari tuliyoisikia kwake Yesu na tunayowahubirieni ndiyo hii: Mungu ni mwanga
na hamna giza lolote ndani yake.
6 Tukisema
kwamba tuna umoja naye,na papo hapo twaishi gizani, tutakuwa tumesema uongo kwa
maneno na matendo.
7 Lakini
tukiishi katika mwanga, kama naye alivyo katika mwanga, basi tutakuwa na umoja
sisi kwa sisi, na damu yake Yesu Kristo, Mwanae, inatutakasa dhambi zote.
8 Tukisema
kwamba hatuna dhambi, tunajidanganya wenyewe na ukweli haumo ndani yetu.
9 Lakini
tukiziungama dhambi zetu, basi Mungu ni mwaminifu na mwadilifu, naye
atatusamehe dhambi zetu na kututakasa na uovu wote.
10
Tukisema kwamba hatujatenda dhambi, tutakuwa tumemfanya Mungu mwongo, na neno
lake halimo ndani yetu.
|