3 John
Chapter 1
1 Mimi
mzee nakuandikia wewe Gayo, rafiki yangu, ninayekupenda kweli.
2 Mpenzi
wangu, nakutakia mafanikio mema ya kila aina; nakutakia afya njema ya mwili
kama ulivyo nayo rohoni.
3
Nimefurahi sana ndugu kadhaa walipofika hapa, wakaiambia juu ya uaminifu wako
kuhusu ukweli; naam, wewe unaishi daima katika ukweli.
4 Hakuna
kitu kinachonifurahisha zaidi kuliko kusikia kwamba watoto wangu wanaishi
katika ukweli.
5 Mpenzi
wangu, wewe ni mwaminifu kila mara unapowahudumia ndugu, hata kama ni wageni.
6 Ndugu
hao wamelieleza kanisa hapa habari za upendo wako. Tafadhali uwasaidie
waendelee na safari yao kwa namna itakayompendeza Mungu,
7 Maana
wanaanza safari yao katika utumishi wa Kristo bila kupokea msaada wowote kutoka
kwa watu wasioamini.
8 Basi,
sisi tunapaswa kuwasaidia watu hawa, ili nasi tupate kushiriki katika kazi yao
kwa ajili ya ukweli.
9
Niliandika barua fupi kwa hilo kanisa; lakini Diotrefe, ambaye hupenda kuwa
kiongozi wao, hataki kabisa kunisikiliza.
10 Basi,
nitakapokuja nitayafichua mambo yote anayofanya, maneno mabaya anayotutolea na
uongo anaosema juu yetu. Isitoshe, yeye hukataa kuwakaribisha hao ndugu walio
safarini, na hata huwazuia watu wengine wanaotaka kuwakaribisha, na hujaribu kuwafukuzia
nje ya kanisa.
11 Mpenzi
wangu, usifuate mfano mbaya, bali mfano mwema. Kila atendaye mema ni wa Mungu;
lakini anayetenda mabaya hajapata kumwona Mungu.
12 Kila
mtu anamsifu Demetrio; naam, ukweli wenyewe unamsifu. Nasi pia tunatoa ushahidi
wetu juu yake, nawe wajua kwamba tunachosema ni kweli.
13 Ninayo
bado mengi ya kukwambia, lakini sipendi kuyaandika kwa kalamu na wino.
14
Natumaini kukuona karibuni na hapo tutazungumza ana kwa ana.
15
Nakutakia amani. Rafiki zako wanakusalimu. Wasalimu rafiki zetu wote kila mmoja
binafsi.
|