Chapter 20
1 Kisha
nikamwona malaika mmoja anashuka kutoka mbinguni akiwa na ufunguo wa kuzimu na
mnyororo mkubwa mkononi mwake.
2
Akalikamata lile joka - nyoka wa kale, yaani Ibilisi au Shetani - akalifunga
kwa muda wa miaka elfu moja.
3 Malaika
akalitupa Kuzimu, akaufunga mlango wa kuingilia huko na kuutia mhuri ili
lisiweze tena kuyapotosha mataifa mpaka hapo miaka elfu moja itakapotimia.
Lakini baada ya miaka hiyo ni lazima lifunguliwe tena, lakini kwa muda mfupi
tu.
4 Kisha
nikaona viti vya enzi na watu walioketi juu yake; watu hao walipewa mamlaka ya
hukumu. Niliona pia roho za wale waliokuwa wamenyongwa kwa sababu ya kumtangaza
Yesu na kwa sababu ya neno la Mungu. Hawa hawakumwabudu yule mnyama na sanamu
yake, wala hawakupigwa alama yake juu ya paji za nyuso zao, au juu ya mikono yao.
Walipata tena uhai, wakatawala pamoja na Kristo kwa muda wa miaka elfu moja.
5 (Wale
wengine waliokufa hawakupata uhai mpaka miaka elfu moja itimie.) Huu ndio
ufufuo wa kwanza.
6
Wameneemeka sana, tena heri yao wote wanaoshiriki ufufuo huu wa kwanza. Kifo
cha pili hakitakuwa na nguvu juu yao; watakuwa makuhani wa Mungu na wa Kristo,
na watatawala pamoja naye kwa miaka elfu moja.
7 Wakati
miaka elfu mia moja itakapotimia, Shetani atafunguliwa kutoka gerezani mwake.
8 Basi,
atatoka nje, ataanza kuyapotosha mataifa yote yaliyotawanyika kila mahali
duniani, yaani Gogu na Magogu. Shetani atawakusanya pamoja kwa ajili ya vita;
nao watakuwa wengi kama mchanga wa pwani.
9 Walitawanyika
katika nchi yote, wakaizunguka kambi ya watu wa Mungu na mji wa Mungu aupendao.
Lakini moto ulishuka kutoka mbinguni, ukawaangamiza.
10
Ibilisi, aliyekuwa anawapotosha, akatupwa ndani ya ziwa linalowaka moto wa
kiberiti, walimo yule mnyama na yule nabii wa uongo, nao watateswa mchana na
usiku, milele na milele.
11 Kisha
nikaona kiti cha enzi kikubwa cheupe, na yule aketiye juu yake. Dunia na mbingu
vikatoweka mbele ya macho yake, na havikuonekana tena.
12 Kisha
nikawaona watu wakubwa na wadogo, wamesimama mbele ya kiti cha enzi, na vitabu
vikafunguliwa. Halafu kitabu kingine, yaani kitabu cha uzima, kikafunguliwa
pia. Wafu wakahukumiwa kadiri ya matendo yao, kama ilivyoandikwa ndani ya
vitabu hivyo.
13 Bahari
ikawatoa nje wafu waliokuwa ndani yake; kifo na kuzimu vikawatoa nje wafu
waliokuwa ndani yao. Kila mmoja akahukumiwa kufuatana na matendo yake.
14 Kisha
kifo na kuzimu vikatupwa ndani ya ziwa la moto. Ziwa hili la moto ndicho kifo
cha pili.
15 Mtu
yeyote ambaye jina lake halikupatikana limeandikwa katika kitabu cha uzima,
alitupwa katika ziwa la moto.
|