Chapter 17
1 Baada ya
siku sita, Yesu aliwachukua Petro, Yakobo na Yohane nduguye, akaenda nao peke
yao juu ya mlima mrefu.
2 Huko,
wakiwa wanamtazama, akageuka sura, uso wake ukang`aa kama jua na mavazi yake
yakawa meupe kama nuru.
3 Mose na
Eliya wakawatokea, wakawa wanazungumza naye.
4 Hapo
Petro akamwambia Yesu, "Bwana, ni vizuri sana kwamba tupo hapa! Ukipenda nitajenga vibanda vitatu:
kimoja chako, kimoja cha Mose na kimoja cha Eliya."
5
Alipokuwa bado anasema hivyo, wingu jeupe likawafunika, na sauti ikasikika
kutoka katika hilo wingu: "Huyu ni Mwanangu mpendwa, ninayependezwa naye,
msikilizeni."
6
Wanafunzi waliposikia hivyo wakaanguka kifudifudi, wakaogopa sana.
7 Yesu
akawaendea, akawagusa, akasema, "Simameni, msiogope!"
8
Walipoinua macho yao hawakumwona mtu, ila Yesu peke yake.
9 Basi,
walipokuwa wanashuka mlimani, Yesu akawaonya: "Msimwambie mtu mambo
mliyoyaona mpaka Mwana wa Mtu atakapofufuliwa kutoka wafu."
10 Kisha
wanafunzi wakamwuliza, "Mbona walimu wa Sheria wanasema ati ni lazima
kwanza Eliya aje?"
11 Yesu
akawajibu, "Kweli, Eliya atakuja kutayarisha mambo yote.
12 Lakini
nawaambieni, Eliya amekwisha kuja nao hawakumtambua, bali walimtendea jinsi
walivyotaka. Mwana wa Mtu atateswa vivyo hivyo mikononi mwao."
13 Hapo
hao wanafunzi wakafahamu kwamba alikuwa akiwaambia juu ya Yohane mbatizaji.
14
Walipojiunga tena na ule umati wa watu, mtu mmoja alimwendea Yesu, akampigia
magoti,
15
akasema, "Mheshimiwa, mwonee huruma mwanangu kwa kuwa ana kifafa, tena
anateseka sana; mara nyingi yeye huanguka motoni na majini.
16
Nilimleta kwa wanafunzi wako lakini hawakuweza kumponya."
17 Yesu
akajibu, "Enyi kizazi kisicho na imani, kilichopotoka! Nitakaa nanyi mpaka
lini? Nitawavumilia ninyi mpaka lini? Mleteni hapa huyo mtoto."
18 Basi,
Yesu akamkemea huyo pepo, naye akamtoka, na yule mtoto akapona wakati huohuo.
19 Kisha
wanafunzi wakamwendea Yesu kwa faragha, wakamwuliza, "Kwa nini sisi
hatukuweza kumtoa yule pepo?"
20 Yesu
akawajibu, "Kwa sababu ya imani yenu haba. Nawaambieni kweli, kama tu
mkiwa na imani, hata iwe ndogo kama mbegu ya haradali, mtaweza kuuambia mlima
huu: `Toka hapa uende pale,` nao utakwenda. Hakuna chochote ambacho
hakingewezekana kwenu."*fg* kuondolewa ila kwa sala na kufunga."
21 missing
22
Walipokuwa pamoja huko Galilaya, Yesu aliwaambia, "Mwana wa Mtu
atakabidhiwa kwa watu.
23
Watamuua, lakini siku ya tatu atafufuliwa." Wanafunzi wakahuzunika mno.
24
Walipofika Kafarnaumu watu wenye kukusanya fedha ya zaka ya Hekalu walimwendea
Petro, wakamwuliza, "Je, mwalimu wenu hulipa fedha ya zaka?"
25 Petro
akajibu, "Naam, hulipa." Basi, Petro alipoingia ndani ya nyumba,
kabla hata hajasema neno, Yesu akamwuliza, "Simoni, wewe unaonaje? Wafalme
wa dunia hukusanya ushuru au kodi kutoka kwa kina nani? Kutoka kwa wananchi ama
kutoka kwa wageni?"
26 Petro
akajibu, "Kutoka kwa wageni." Yesu akamwambia, "Haya
basi, wananchi hawahusiki.
27 Lakini kusudi tusiwakwaze, nenda ziwani ukatupe ndoana;
chukua samaki wa kwanza atakayenaswa, fungua kinywa chake, na ndani utakuta
fedha taslimu ya zaka. Ichukue ukawape kwa ajili yangu na kwa ajili yako."
|