Chapter 21
1 Yesu na wanafunzi wake walipokaribia Yerusalemu na kufika
Bethfage katika mlima wa Mizeituni, aliwatuma wanafunzi wake wawili,
2 akawaambia, "Nendeni hadi kijiji kilicho mbele yenu
na mtamkuta punda amefungwa na mtoto wake. Wafungueni mkawalete kwangu.
3 Kama mtu akiwauliza sababu, mwambieni, `Bwana
anawahitaji,` naye atawaachieni mara."
4 Jambo hili lilifanyika ili yale yaliyosemwa na nabii
yatimie:
5 "Uambieni mji wa Sioni: Tazama, Mfalme wako
anakujia! Ni mpole na amepanda
punda, mwana punda, mtoto wa punda."
6 Hivyo,
wale wanafunzi walienda wakafanya kama Yesu alivyowaagiza.
7
Wakamleta yule punda na mtoto wake, wakatandika nguo zao juu yao na Yesu
akaketi juu yake.
8 Umati
mkubwa wa watu ukatandaza nguo zao barabarani, na watu wengine wakakata matawi
ya miti wakayatandaza barabarani.
9 Makundi
ya watu waliomtangulia na wale waliomfuata wakapaaza sauti: "Hosana Mwana
wa Daudi! Abarikiwe huyo ajaye kwa jina la Bwana! Hosana Mungu juu
mbinguni!"
10 Yesu
alipokuwa anaingia Yerusalemu, mji wote ukajaa ghasia. Watu wakawa wanauliza,
"Huyu ni nani?"
11 Watu
katika ule umati wakasema, "Huyu ni nabii Yesu, kutoka Nazareti katika
mkoa wa Galilaya."
12 Basi,
Yesu akaingia Hekaluni, akawafukuza nje watu waliokuwa wanauza na kununua vitu
ndani ya Hekalu; akazipindua meza za wale waliokuwa wanavunja fedha, na viti
vya wale waliokuwa wanauza njiwa.
13
Akawaambia, "Imeandikwa katika Maandiko Matakatifu: `Nyumba yangu itaitwa
nyumba ya sala.` Lakini ninyi mmeifanya kuwa pango la wanyang`anyi."
14 Vipofu
na vilema walimwendea huko Hekaluni, naye Yesu akawaponya.
15 Basi,
makuhani wakuu na walimu wa Sheria walipoyaona maajabu aliyoyafanya Yesu, na
pia watoto walipokuwa wanapaaza sauti zao Hekaluni wakisema: "Sifa kwa
Mwana wa Daudi," wakakasirika.
16 Hivyo
wakamwambia, "Je, husikii wanachosema?" Yesu akawajibu, "Naam,
nasikia! Je hamjasoma Maandiko haya Matakatifu? `Kwa vinywa vya watoto wadogo
na wanyonyao unajipatia sifa kamilifu."`
17 Basi,
akawaacha, akatoka nje ya mji na kwenda Bethania, akalala huko.
18 Yesu
alipokuwa anarudi mjini asubuhi na mapema, aliona njaa.
19 Akauona
mtini mmoja kando ya njia, akauendea; lakini aliukuta hauma chochote ila majani
matupu. Basi akauambia, "Usizae tena matunda milele!" Papo hapo huo
mtini ukanyauka.
20
Wanafunzi walipouona walishangaa wakisema, "Kwa nini mtini huu umenyauka
ghafla?"
21 Yesu
akawajibu, "Kweli nawaambieni, kama mkiwa na imani bila kuwa na mashaka,
mnaweza si tu kufanya hivyo, bali hata mkiuambia mlima huu: `Ng`oka ukajitose
baharini,` itafanyika hivyo.
22 Na
mkiwa na imani, chochote mtakachoomba katika sala, mtapata."
23 Yesu
aliingia Hekaluni, akawa anafundisha. Alipokuwa akifundisha, makuhani wakuu na
wazee wa watu wakamwuliza, "Unafanya mambo haya kwa mamlaka gani? Nani
amekupa mamlaka haya?"
24 Yesu
akawajibu, "Na mimi nitawaulizeni swali moja; mkinijibu, basi nami
nitawaambieni ninafanya mambo haya kwa mamlaka gani.
25 Je,
mamlaka ya Yohane ya kubatiza yalitoka kwa nani? Je, yalitoka mbinguni ama kwa
watu?" Lakini wakajadiliana wao kwa wao hivi: "Tukisema, `Yalitoka
mbinguni`, atatuuliza, `Basi, mbona hamkumsadiki?`
26 Na
tukisema, `Yalitoka kwa watu,` tunaogopa umati wa watu maana wote wanakubali
kwamba Yohane ni nabii."
27 Basi,
wakamjibu, "Hatujui!" Naye Yesu akawaambia, "Nami pia
sitawaambieni ninafanya mambo haya kwa mamlaka gani.
28
"Ninyi mnaonaje; mtu mmoja alikuwa na wana wawili. Akamwambia yule wa
kwanza, `Mwanangu, leo nenda ukafanye kazi katika shamba la mizabibu.`
29 Yule
kijana akamwambia, `Sitaki!` Lakini baadaye akabadili nia, akaenda kufanya
kazi.
30 Yule
baba akamwambia mtoto wake wa pili vivyo hivyo, naye akamjibu, `Naam baba!`
Lakini hakwenda kazini.
31 Je, ni
nani kati ya hawa wawili aliyetimiza matakwa ya baba yake?" Wakamjibu,
"Yule mtoto wa kwanza." Basi, Yesu akawaambia, "Kweli
nawaambieni, watoza ushuru na waasherati wataingia katika Ufalme wa Mungu kabla
yenu.
32 Maana
Yohane alikuja kwenu akawaonyesha njia njema ya kuishi, nanyi hamkumwamini; lakini
watoza ushuru na waasherati walimwamini. Hata baada ya kuona hayo yote ninyi
hamkubadili mioyo yenu, na hamkusadiki."
33 Yesu
akasema, "Sikilizeni mfano mwingine. Mtu mmoja mwenye nyumba alilima
shamba la mizabibu; akalizungushia ukuta, akachimba kisima cha kusindikia
divai, akajenga humo mnara pia. Kisha akalikodisha kwa wakulima, akasafiri
kwenda nchi ya mbali.
34 Wakati
wa mavuno ulipofika, aliwatuma watumishi wake kwa wale wakulima, ili wakachukue
sehemu ya mavuno yake.
35 Wale
wakulima wakawakamata hao watumishi; mmoja wakampiga, mwingine wakamwua na
mwingine wakampiga mawe.
36 Huyo
mtu akawatuma tena watumishi wengine, wengi kuliko wa safari ya kwanza. Wale
wakulima wakawatendea namna ileile.
37
Mwishowe akamtuma mwanawe huku akifikiri: `Watamheshimu mwanangu.`
38 Lakini
wale wakulima walipomwona mwanawe wakasemezana wao kwa wao: `Huyu ndiye mrithi;
na tumuue ili tuuchukue urithi wake!`
39 Basi,
wakamkamata, wakamtoa nje ya lile shamba la mizabibu, wakamwua.
40
"Sasa, huyo mwenye shamba la mizabibu atakapokuja, atawafanyaje hao
wakulima?"
41 Wao
wakamjibu, "Atawaangamiza vibaya hao waovu, na lile shamba atawapa
wakulima wengine ambao watampa sehemu ya mavuno wakati wa mavuno."
42 Hapo
Yesu akawaambia, "Je, hamkusoma jambo hili katika Maandiko Matakatifu?
`Jiwe walilokataa waashi sasa limekuwa jiwe kuu la msingi. Bwana ndiye
aliyefanya jambo hili, nalo ni la ajabu sana kwetu!`
43
"Kwa hiyo nawaambieni, Ufalme wa Mungu utaondolewa kwenu na kupewa watu wa
mataifa mengine wenye kutoa matunda yake."*fi* likimwangukia mtu yeyote,
litamponda."
44 missing
45
Makuhani wakuu na Mafarisayo waliposikia hiyo mifano yake walitambua kwamba
alikuwa anawasema wao.
46 Kwa
hiyo wakawa wanatafuta njia ya kumtia nguvuni, lakini waliwaogopa watu kwa
sababu wao walimtambua yeye kuwa nabii.
|