Mfano wa karamu ya arusi
\r
\is (Luka 14:15-24)
\ie
1 Yesu
alisema nao tena kwa kutumia mifano:
2 "Ufalme wa mbinguni umefanana na mfalme aliyemwandalia
mwanawe
karamu ya arusi.
3 Basi, akawatuma watumishi kuwaita walioalikwa waje arusini,
lakini
walioalikwa hawakutaka kufika.
4 Akawatuma tena watumishi wengine, akisema, <Waambieni
wale
walioalikwa: karamu yangu iko tayari sasa; fahali wangu na ng'ombe
wanono wamekwisha chinjwa; kila kitu ni tayari, njoni arusini.>
5 Lakini wao hawakujali, wakaenda zao; mmoja shambani kwake,
mwingine kwenye shughuli zake,
6 na wengine wakawakamata wale watumishi wakawatukana,
wakawaua.
7 Yule mfalme akakasirika, akawatuma askari wake
wakawaangamize
wauaji hao na kuuteketeza mji wao.
8 Kisha akawaambia watumishi wake: <Karamu ya arusi iko
tayari
kweli, lakini walioalikwa hawakustahili.
9 Basi, nendeni kwenye barabara na wowote wale mtakaowakuta
waiteni
waje arusini.>
10 Wale watumishi wakatoka, wakaenda njiani, wakawaleta watu
wote,
wabaya na wema. Nyumba ya arusi ikajaa wageni.
11
"Mfalme alipoingia kuwaona wageni, akamwona mtu mmoja ambaye
hakuvaa mavazi ya arusi.
12 Mfalme akamwuliza, <Rafiki, umeingiaje hapa bila vazi la
arusi?>
Lakini yeye akakaa kimya.
13 Hapo mfalme akawaambia watumishi, <Mfungeni miguu na
mikono
mkamtupe nje gizani; huko atalia na kusaga meno.">
14 Yesu akamaliza kwa kusema, "Wengi wamealikwa, lakini
wachache
wameteuliwa."
Kulipa kodi kwa Kaisari
\r
\is (Marko 12:13-17; Luka 20:20-26)
\ie
15 Kisha,
Mafarisayo wakaenda zao, wakashauriana jinsi ya kumnasa
Yesu kwa maneno yake.
16 Basi, wakawatuma wafuasi wao pamoja na wafuasi wa kikundi
cha
Herode. Wakamwuliza, "Mwalimu, tunajua kwamba wewe ni mtu mwaminifu, na
kwamba wafundisha njia ya Mungu kwa uaminifu; humwogopi mtu yeyote,
maana cheo cha mtu si kitu kwako.
17 Haya, twambie maoni yako. Je, ni halali au la, kulipa
Kaisari?"
18 Lakini Yesu alitambua uovu wao, akawaambia, "Enyi
19 Nionyesheni fedha ya kulipia kodi." Nao wakamtolea
sarafu ya
fedha. sarafu ya fedha.
20 Basi, Yesu akawauliza, "Sura na chapa hii ni ya
nani?"
21 Wakamjibu, "Ni vya Kaisari." Hapo Yesu
akawaambia, "Basi,
mpeni Kaisari yaliyo yake Kaisari, na Mungu yaliyo yake Mungu."
22 Waliposikia hivyo wakashangaa; wakamwacha, wakaenda zao.
Kuhusu ufufuo
\r
\is (Marko 12:18-27; Luka 20:27-40)
\ie
23 Siku
hiyo, baadhi ya Masadukayo walimwendea Yesu. Hao ndio wale
wasemao kwamba wafu hawafufuki.
24 Basi, wakamwambia, "Mwalimu, Mose alisema mtu aliyeoa
akifa bila
kuacha watoto, lazima ndugu yake amwoe huyo mama mjane, amzalie ndugu
yake watoto.
25 Sasa, hapa petu palikuwa na ndugu saba. Wa kwanza alioa
kisha
akafa bila kujaliwa watoto, akamwachia ndugu yake huyo mke wake mjane.
26 Ikawa vivyo hivyo kwa ndugu wa pili, na wa tatu, mpaka wa
saba.
27 Baada ya ndugu hao wote kufa, akafa pia yule mama.
28 Je, siku wafu watakapofufuka mama huyo atakuwa mke wa nani
miongoni mwa wale ndugu saba? Maana Wote saba walimwoa."
29 Yesu
akawajibu, "Kweli mmekosea kwa sababu hamjui Maandiko
Matakatifu wala nguvu ya Mungu!
30 Maana wafu watakapofufuliwa hawataoa wala kuolewa, watakuwa
kama
malaika mbinguni.
31 Lakini kuhusu suala la wafu kufufuka, hamjasoma yale
aliyowaambieni Mungu?
32 Aliwaambia, <Mimi ni Mungu wa Abrahamu, Isaka na
Yakobo!> Basi,
yeye si Mungu wa wafu, bali ni Mungu wa walio hai."
33 Ule umati wa watu uliposikia hivyo ukayastaajabia
mafundisho
yake.
Amri kuu
\r
\is (Marko 12:28-34; Luka 10:25-28)
\ie
34 Mafarisayo waliposikia kwamba Yesu alikuwa
amewanyamazisha
Masadukayo, wakakutana pamoja.
35 Mmoja wao, mwanasheria, akamwuliza Yesu kwa kumjaribu,
36 "Mwalimu, ni amri ipi iliyo kuu katika Sheria ya
Mose?"
37 Yesu akamjibu, "<Mpende Bwana Mungu wako kwa moyo
wako wote, kwa
roho yako yote na kwa akili yako yote.>
38 Hii ndiyo amri kuu ya kwanza.
39 Ya pili inafanana na hiyo: <Mpende jirani yako kama
unavyojipenda
wewe mwenyewe.>
40 Sheria yote ya Mose na mafundisho ya manabii vinategemea
amri
hizi mbili."
Kuhusu Mwana wa Daudi
\r
\is (Marko 12:35-37; Luka 20:41-44)
\ie
41 Mafarisayo walipokusanyika pamoja, Yesu
aliwauliza,
42 "Ninyi mwaonaje juu ya Kristo? Je, ni mwana wa
nani?"
Wakamjibu, "Wa Daudi."
43 Yesu akawaambia, "Basi, inawezekanaje kwamba kwa nguvu
ya Roho
Mtakatifu Daudi anamwita yeye Bwana? Maana alisema:
44 <Bwana alimwambia Bwana wangu:
keti upande wangu wa kulia,
mpaka niwaweke adui zako chini ya miguu
yako.>
\m
45 Basi, ikiwa Daudi anamwita Kristo <Bwana,> anawezaje
kuwa
mwanawe?"
46 Hakuna mtu yeyote aliyeweza kumjibu neno. Na tangu siku
hiyo
hakuna aliyethubutu tena kumwuliza swali.
\fr 22:44
\f Taz Zab 110:1
|