Chapter 6
1 Yesu
aliondoka hapo akaenda katika kijiji chake, akifuatwa na wanafunzi wake.
2 Siku ya
Sabato ilipofika, alianza kufundisha katika sunagogi. Wengi waliomsikia
walishangaa, wakasema, "Je, ameyapata wapi mambo haya? Ni hekima gani hii
aliyopewa? Tena, anatendaje maajabu haya anayoyafanya?
3 Je, huyu
si yule seremala mwana wa Maria, na ndugu yao kina Yakobo, Yose, Yuda na
Simoni; Je, dada zake si wanaishi papa hapa kwetu?" Basi, wakawa na
mashaka naye. ic\is Ndani ya Sunagogi (Marko 6:2)\ie
4 Yesu
akawaambia, "Nabii hakosi heshima isipokuwa katika nchi yake, kwa jamaa
zake na nyumbani mwake."
5 Hakuweza
kutenda miujiza hapo, ila aliwawekea mikono wagonjwa wachache, akawaponya.
6
Alishangaa sana kwa sababu ya kutoamini kwao. Kisha Yesu alivitembelea vijiji
vya pale karibu akiwafundisha watu.
7 Aliwaita
wale wanafunzi kumi na wawili, akaanza kuwatuma wawiliwawili. Aliwapa uwezo wa
kuwatoa pepo wachafu,
8 na
kuwaamuru, "Msichukue chochote mnapokwenda isipokuwa fimbo tu. Msichukue
mkate, wala mkoba, wala fedha kibindoni.
9 Vaeni
viatu lakini msivae kanzu mbili."
10 Tena
aliwaambia, "Popote mtakapokaribishwa nyumbani, kaeni humo mpaka
mtakapoondoka mahali hapo.
11 Mahali
popote ambapo watu watakataa kuwakaribisheni au kuwasikiliza, ondokeni hapo na
kuyakung`uta mavumbi miguuni mwenu kama onyo kwao."
12 Basi,
wakaondoka, wakahubiri watu watubu.
13
Waliwafukuza pepo wengi wabaya; wakawapaka mafuta wagonjwa wengi, wakawaponya.
14 Basi,
mfalme Herode alisikia juu ya hayo yote, maana sifa za Yesu zilienea kila
mahali. Baadhi ya watu walikuwa wakisema, "Yohane Mbatizaji amefufuka
kutoka wafu, ndiyo maana nguvu za miujiza zinafanya kazi ndani yake."
15 Wengine
walisema, "Mtu huyu ni Eliya." Wengine walisema, "Huyu ni nabii
kama mmojawapo wa manabii wa kale."
16 Lakini
Herode alipopata habari hizi alisema, "Huyu ni Yohane! Nilimkata kichwa,
lakini amefufuka."
17 Hapo
awali Herode mwenyewe alikuwa ameamuru Yohane atiwe nguvuni, akamfunga
gerezani. Herode alifanya hivyo kwa sababu ya Herodia ambaye Herode alimwoa
ingawaje alikuwa mke wa Filipo, ndugu yake.
18 Yohane
alikuwa amemwambia Herode, "Si halali kwako kumchukua mke wa ndugu
yako."
19 Basi
Herodia alimchukia sana Yohane, akataka kumwua, asiweze.
20 Herode
alimwogopa Yohane kwa maana alijua kwamba yeye ni mtu mwema na mtakatifu, na
hivyo akamlinda. Herode alipenda kumsikiliza Yohane, ingawaje baada ya
kumsikiliza, alifadhaika sana.
21
Ikapatikana nafasi, wakati wa sikukuu ya kuzaliwa kwake Herode. Herode
aliwafanyia karamu wazee wa baraza lake, majemadari na viongozi wa Galilaya.
22 Basi,
binti yake Herodia aliingia, akacheza, akawafurahisha sana Herode na wageni
wake. Mfalme akamwambia huyo msichana, "Niombe chochote utakacho, nami
nitakupa."
23 Tena
akamwapia, "Chochote utakachoniomba, nitakupa: hata ikiwa ni nusu ya
ufalme wangu."
24 Hapo
huyo msichana akatoka, akamwuliza mama yake, "Niombe nini?" Naye
akamjibu, "Kichwa cha Yohane mbatizaji."
25
Msichana akamrudia mfalme mbio akamwomba, "Nataka unipe sasa hivi katika
sinia kichwa cha Yohane mbatizaji."
26 Mfalme
akahuzunika sana, lakini kwa sababu ya kiapo chake, na kwa ajili ya wale wageni
wake karamuni, hakutaka kumkatalia.
27 Basi,
mfalme akamwamuru askari kukileta kichwa cha Yohane. Askari akaenda, akamkata
kichwa Yohane mle gerezani,
28
akakileta katika sinia, akampa msichana naye msichana akampa mama yake.
29
Wanafunzi wa Yohane walipopata habari, walikwenda wakachukua mwili wake,
wakauzika kaburini.
30 Wale
mitume walirudi, wakakusanyika mbele ya Yesu wakamwarifu yote waliyotenda na
kufundisha.
31 Alisema
hivyo kwa kuwa kulikuwa na watu wengi mno walikuwa wanafika hapo na kuondoka
hata Yesu na wanafunzi wake hawakuweza kupata nafasi ya kula chakula. Basi,
Yesu akawaambia, "Twendeni peke yetu mahali pa faragha kula chakula,
mkapumzike kidogo."
32 Basi,
Wakaondoka peke yao kwa mashua, wakaenda mahali pa faragha.
33 Lakini
watu wengi waliwaona wakienda, wakawatambua. Hivyo wengi wakatoka katika kila
mji, wakakimbilia huko Yesu na wanafunzi wake walikokuwa wanakwenda,
wakawatangulia kufika.
34 Waliposhuka
pwani, Yesu aliona umati mkubwa wa watu, akawahurumia, kwa sababu walikuwa kama
kondoo wasio na mchungaji. Akaanza kuwafundisha mambo mengi.
35 Saa za
mchana zilikwisha pita. Basi, wanafunzi wakamwendea Yesu, wakamwambia,
"Hapa ni nyikani, na sasa kunakuchwa.
36
Afadhali uwaage watu waende mashambani na katika vijiji vya jirani, wanunue
chakula."
37 Lakini
Yesu akawaambia, "Wapeni ninyi chakula." Nao wakamwuliza, "Je,
twende kununua mikate kwa fedha dinari mia mbili, na kuwapa chakula?"
38 Yesu
akawauliza, "Mnayo mikate mingapi? Nendeni mkatazame." Walipokwisha
tazama, wakamwambia, "Kuna mikate mitano na samaki wawili." ic\is
Mikate na samaki (Marko 6:38)\ie
39 Basi,
Yesu akawaamuru wanafunzi wawaketishe watu wote makundimakundi penye nyasi.
40 Nao
wakaketi makundimakundi ya watu mia moja na ya watu hamsini.
41 Kisha
Yesu akaitwaa ile mikate mitano na wale samaki wawili, akatazama juu mbinguni,
akamshukuru Mungu, akaimega mikate, akawapa wanafunzi wake wawagawie watu. Na
wale samaki wawili pia akawagawia wote.
42 Watu
wote wakala, wakashiba.
43
Wakaokota mabaki ya mikate na samaki pia, wakajaza vikapu kumi na viwili.
44 Nao
waliokula hiyo mikate walikuwa wanaume elfu tano.
45 Mara
Yesu akawaamuru wanafunzi wake wapande mashua, wamtangulie kwenda Bethsaida,
ng`ambo ya ziwa, wakati yeye anauaga umati wa watu.
46 Baada
ya kuwaaga watu alikwenda mlimani kusali.
47
Ilipokuwa jioni, mashua ilikuwa katikati ya ziwa, naye alikuwa peke yake katika
nchi kavu.
48 Basi,
akawaona wanafunzi wake wakitaabika kwa kupiga makasia, maana upepo ulikuwa
unawapinga. Karibu na mapambazuko, Yesu aliwaendea akitembea juu ya maji.
Alitaka kuwapita.
49 Lakini
walimwona akitembea juu ya maji, wakadhani ni mzimu, wakapiga yowe.
50 Maana wote walipomwona waliogopa sana. Mara Yesu akasema
nao, "Tulieni, ni mimi. Msiogope!"
51 Kisha akapanda mashuani walimokuwa, na upepo ukatulia.
Nao wakashangaa sana.
52 maana hawakuwa bado wameelewa maana ya ile mikate. Akili
zao zilikuwa bado zimepumbazika.
53 Walivuka ziwa, wakafika nchi ya Genesareti, wakatia
nanga.
54 Walipotoka mashuani, mara watu wakamtambua Yesu.
55 Basi, kwa haraka wakazunguka katika nchi ile yote,
wakaanza kuwachukua wagonjwa wamelala juu ya mikeka yao, wakawapeleka kila
mahali waliposikia Yesu yupo.
56 Kila mahali Yesu alipokwenda, vijijini, mijini, au
mashambani, watu waliwaweka wagonjwa uwanjani, wakamsihi waguse walau pindo la
vazi lake. Nao wote waliomgusa walipona.
|