Wapendwa
Dada na Kaka,
Mwaka huu,
adhimisho la kwaresma, ni la kipekee;linatokea wakati wa uongofu na upatanisho
lina hali ya pekee likitokea wakati wa Jubilei Kuu ya Mwaka 2000. Kwa kweli
wakati wa Kwaresma ni wakati wa kilele cha safari ya kuongoka na kupatanishwa
ambao ni Jubilei, mwaka wa Bwana, unatoa fursa kwa waaminifu ili wazaliwe upya
katika Kristo na kutangaza uponyaji wake wa miujiza kwa hamu kubwa katika
millenia mpya.
Kwaresma inawasaidia Wakristo
kuingia kwa undani zaidi katika, " siri iliyofichika kwa zama
zote"(Ef 3:9) Inawaongoza Wakristo kukutana ana kwa na Neno la Mungu na
kuwataka kuachana na ubinafsi ili wapate kuongozwa na Roho Mtakatifu
Tulikuwa wafu kupitia dhambi(Efe
2:5). Ndivyo Mtakatifu Paulo anavyoielezea hali ya ilivyo kwa mtu asiye na
Kristo.
Ndiyo maana Mwana wa Mungu
alijifanya mtu, na kuungama na kuwatoa katika utumwa wa dhambi na mauti.
Huu ndio utumwa anao kutana nao
kila siku kwa namna ulivyo na mizizi ndani ya moyo wake.(Mat 7:11). Wakati
mwingine utumwa huo unajionesha wenyewe kwa njia zisizo za kawaida, kama
ilivyotokea katika matukio makubwa ya karne ya ishirini, yaliyogusa kwa undani
maisha ya jumuia na watu wasihesabika, Waathirika wa vurugu za kikatili,
kuhamishwa kinguvu katika makazi,uangamizaji wa watu na kunyimwa haki zao za
msingi za kibinadamu.haya ndiyo maovu yanayo unyanyasa ubinadamu hadi
leo.katika maisha ya kila siku, pia tunashuhudia aina mbalimbali za utapeli,
chuki, mauaji na udanganyifu ambao mwanadamu ndiyo chanzo chake na ndiye
muathirika pia.
Ubinadamu unakabiliwa na dhambi.
Hali mbaya ya binadamu inatukumbusha kilio alichotoa Mtume Paulo kwa mataifa:
"Hakuna mwenye haki hata mmoja" (Rum 3: 10; Zab. 14: 3)
Kwa sura ya giza la dhambi na
kushindwa kwa binadamu kujiokoa mwenyewe, ndipo inapotokea katika mwonekano
wote, kazi ya ukombozi wa Kristo. "Ambaye Mungu amekwisha muweka awe
upatanisho kwa njia ya imani katika damu yake ili aoneshe haki yake" (Rum.
3:25)Kristo ni Mwanakondoo wa Mungu aliyechukua dhambi za ulimwengu.(Yn. 1:29).
"Tena alipoonekana ana umbo kama mwanadamu, alijinyenyekeza akawa mtii
hata mauti, naam, mauti ya msalaba."(Flp. 2:8)ili kumkomboa mwanadamu toka
utumwa wa dhambi na kumrudisha katika asili ya ubinadamu wake kama Mwana wa Mungu.
Hili ni Fumbo la Pasaka ambalo
kwalo, tunazaliwa upya.Hapa ni kama utaratibu wa Pasaka unavyosema, "Kifo
kilishindana na maisha, shindano lililoisha kimaajabu."
Mababa wa Kanisa wanakiri kwamba
katika Kristo Yesu, shetani ambaye huvamia ubinadamu na kuushikamanisha na
kifo, mtu huwekwa huru kwa uwezo wa ufufuko.
Katika Bwana Mfufuka, nguvu za
kifo huangamizwa na kupitia imani, mtu huingia na Mungu katika Jumuia.
Kwa waamini, maisha ya Kimungu
hutolwa kwa utendaji wa Roho Mtakatifu. "Zawadi ya kwanza kwa
Waamini" (Sala ya Ekaristi IV).
Hivyo, ukombozi uliokamilishwa
msalabani huufanya upya ulimwengu na kuleta upatanisho kati ya mungu na mtu, na
kati ya mtu na mtu.
Jubilei ni wakati wa neema ambapo
tunaalikwa kujifunua kwa namna ya pekee kwa huruma wa Baba, ambaye kupitia
Mwana, amemfikia mtu na kutuletea upatanisho ambao ni zawadi kubwa aliyotupa
kristo.
Kwa hiyo, mwaka huu, si tu kwa
Wakristo, bali pia kwa watu wenye mapenzi mema, unapaswa kuwa wakati mwafaka wa
kushuhudia uwezo wa Mungu katika kupenda na kusamehe.
Mungu humhurumia yeyote anayekuwa
tayari kupokea huruma hiyo hata kwa aliye mbali, na mwenye mashaka.Watu wa
nyakati zetu waliochoshwa na matumaini ya uongo, wanapewa nafasi kupitia kwenye
njia ya ukamilifu wa maisha.
Kwa mtazamo huu, Kwaresma ya
Mwaka Mtakatifu wa 2000 ni"wakati uliokubalika-siku ya
Wokovu"(2Kor.6:2)na ni nafasi inayofaa "kupatanishwa na Mungu"
(2Kor.5:20).
Wakati wa Mwaka Mtakatifu, Kanisa
linatoa nafasi mbalimbali kwa mtu binafsi na kwa jumuiya. Kila jimbo
limependekeza maeneo maalumu ambapo waamini wanaweza kwenda ili kushuhudia
uwepo wa Mungu,kwa kutambua madhambi yao kupitia mwanga wake, na kwa Sakramenti
ya Upatanisho, waingie katika njia mpya ya maisha.
Umuhimu wa pekee unahusishwa na
kuhiji katika Nchi Takatifu ya Roma, sehemu mahsusi za kukutana na Mungu
kutokana na umuhimu wake wa kipekee katika historia ya Wokovu.
Tutashindwaje japo kiroho,
kuelekea nchi ambayo miaka elfu mbili iliyopita, ilimshuhudia Bwana akiipita?
Hapo, "Neno alifanyika mwili" (Yn.1:14) na "akazidi kuendelea
katika hekima na kimo,akimpendeza Mungu na wanadamu (Lk.2:25)."hapo,
alikuwa akizunguka katika miji yote akihubiri Habari Njema ya ufalme na kuponya
yote na udhaifu wa kila aina" (Mat 9:35); hapo alikamilisha jukumu
alilopewa na Baba. (Yn.19:30)na kuvuvia Roho Mtakatifu kwa kanisa la Mwanzo.
(Yn.20:22).
Pia, natumaini hasa wakati wa
Kwaresma ya Mwaka 2000, kuhiji katika Nchi Takatifu pale ambapo imani yetu
ilianzia, ili kuadhimisha Jubilei ya miaka elfu mbili ya umwilisho.Ninawaalika
Wakristo wote kuungana nami kwa sala zao wakati mimi mwenyewe katika hatua
mbalimbali zakuhiji, nitaomba msamaha na upatanisho kwa Wanakanisa na watu
wote.
Njia ya kuongoka hutufikisha
katika upatanisho na Mungu na hutuingiza kwenye ukamilifu wa maisha mapya
katika Kristo, maisha ya imani, matumaini na upendo.
Fadhila hizi tatu hujulikana kama
fadhila za "kiteolojia" kwa sababu zinatuelekeza moja kwa moja kwa
mungu katika Fumbo lake. Zimekuwa pia kiini cha mtazamo wa pekee kwa kipindi
cha miaka mitatu ya matayarisho ya Jubilei Kuu. Maadhimisho ya Mwaka Mtakatifu
yana mualika kila Mkristo kuziishi na kuzishuhudia fadhila hizi tatu kwa namna
ya ukamilifu zaidi.
Zaidi ya yote, neema za Jubilei
zinatutaka kuimarisha imani yetu binafsi.Hii inahusisha kuendelea kutangaza
Fumbo la Pasaka ambalo kwalo waamini wanatambua kwamba katika Kristo Msulubiwa
na Mfufuka katika wafu,wamepata Wokovu. Siku hadi siku, wanamtolea maisha yao,
wanakubali kila kitu anachokikusudia Bwana kwa ajili yao na kwa uhakika kwamba
Mungu anawapenda. Imani ni "ndiyo" ya kila mtu kwa Mungu, na ndiyo
"amina" yao.
Kwa Wayahudi, Wakristo na
Waislamu kadhalika, Abrahamu ni mfano, kwa kuziamini ahadi aliifuata sauti ya
Mungu iliyomtaka kuelekea asikokujua. Imani inatusaidia kuzigundua alama za
upendo wa Mungu katika uumbaji,watu, matukio ya historia na zaidi ya yote,
kupitia matendo na ujumbe wa Kristo kadri anavyowaamsha watu kujitafiti wenyewe
na kufikia pale ambapo Fumbo la Upendo wa Mungu kwa kila kiumbe wa Mungu
hudhihirika.
Kupitia neema za Jubilei, Bwana
anatualika pia kuimarisha matumaini yetu. Kwa kweli, wakati wenyewe
unakombolewa katika Kristo na kufungua matarajio ya furaha isiyo na mwisho kwa
muungano kamili na Mungu.Kwa Wakristo, muungano unaashiriwa na matarajio ya
sherehe za milele ambazo hutabiriwa kila siku kwenye meza ya ekaristi
wakitazmia furaha ya milele, "Roho na Bibi harusi wasema Njoo." (Ufu.
22:17)
Wanadumisha matumaini ambayo
huukomboa wakati kutoka hali yake ya kujirudia na kuupa maana yake halisi.
Kupitia fadhila ya matumaini,
Wakristu hushuhudia ukweli kwamba ndani ya uovu wote, historia huzaa mbegu ya
wema ambayo Bwana ataiwezesha kufikia ukamilifu wake. Kwa hiyo Wakristu
wanatazamia katika Milenia mpya kukabliana bila wasiwasi na changamoto na
matazamio ya baadaye kwa uhakika wenye msingi katika imani inayotokana na ahadi
ya Bwana.
Hatimaye, kupitia Jubilei Bwana
anatuomba tuimarishe upendo wetu.
Ufalme ambao Kristo ataufunua
katika ukamilifu wake mwishoni mwa nyakati tayari umejidhihirisha pale ambapo
watu wanaishi kwa kadri ya mapenzi ya Mungu.
Kanisa linaalikwa kushuhudia
amani na upendo ambavyo ni alama pekee za ufalme. Katika jukumu hili jumuiya ya
Kikristo inajua kwamba imani pasipo matendo imekufa.(Yak.2:17).
Hivi kwa upendo, Wakristo
huonyesha upendo wa Mungu kwa mtu, unaojifunua katika Kristo na kudhihirisha
uwepo wa Kristo duniani "mpaka mwisho wa nyakati." Kwa Wakristo,
upendo sio tu kitu cha fikra, bali ni mwendelezo wa uwepo Kristo anayejitoa
mwenyewe.
Wakati wa Kwaresma, tajiri na
maskini wanaalikwa kuuwezesha upendo wa Kristo uwepo kwa matendo mema.
Wakati huu wa mwaka wa Jubilei,
upendo wetu unapaswa kuonekana ukishuhudia upendo wa Kristo kwa ndugu zetu
ambao wanakosa mahitaji muhimu ya maisha, wanaoteseka kwa njaa, magomvi na
dhuluma.
Hii ndiyo njia ya kufanya fikra
za ukombozi na ndugu zionekane katika Maandiko Matakatifu, zionekane kuwa kitu
cha kweli, fikra ambazo mwaka mtakatifu huziweka mbele kwa mara nyingine.
Jubilei ya kizamani ya Kiyahudi
kwa hakika ilitaka kuachiwa huru wafungwa, kufuta madeni na ktoa msaada kwa maskini.
Leo hii aina mpya za utumwa na miundo mibaya ya umaskini huathri idadi kubwa ya
watu, hasa kwenye zile zinazoitwa nchi za dunia ya tatu.
Hiki ni kituo cha wanaoteseka na
kukata tamaa, ambacho lazima kisikike na kupatiwa jawabu kwa wote wanaoipita njia
ya Jubilei. Tutawezaje kuomba neema za Jubilei kama hatujali mahitaji ya
maskini, kama hatujitahidi kuona kwamba wote wanapata mahitaji muhimu kwa
maisha ya kisasa?
Basi Milenia hii iwe wakati ambao
kilio cha ndugu zetu wasio na mahitaji kinasikika na kupatiwa jawabu muafaka.
Ni matumaini yangu kwamba
Wakristo wa ngazi zote watakuwa mstari wa mbele kudumisha jitihada
zitakazopelekea usawa katika ugawanaji rasilimali na kudumisha maendeleo kamili
ya kila mtu.
"Mimi niko pamoja nanyi siku
zote, hata ukamilifu wa dahari." Maneno hayo ya Yesu yanatuhakikishia
kwamba katika kuitangaza na kuiishi Injili ya upendo hatupo peke yetu.
Kwa mara nyingine wakati huu wa
Kwaresma ya mwaka 2000 anatualika tena kumrudia Baba anayetusubiri atuwezeshe
kuwa ishara hai za upendo wake wenye huruma.
Kwa Maria Mama wa wote
wanaoteseka na Mama wa Huruma ya Mungu tunamkabidhi nia zetu na maazimio yetu.
Basi, awe nyota inayong’ara katika safari yetu ya Milenia mpya.
Kwa maneno haya namtakia kila mmoja wenu Baraka za Mungu Mmoja katika Utatu,
Mwanzo na Mwisho wa vitu vyote, ambaye kwake tunamtaka " mpaka mwisho wa
nyakati," wimbo wenyeBaraka na sifa kwa Kristo.
"Kwa njia yake, pamoja naye na ndani yake, katika Umoja wa Roho
mtakatifu unapata heshima na utukufu wote, Baba Mwenyezi, daima na milele. AMINA."
Yohane Paulo ll, Vatican.
|